Wednesday, April 22, 2015

MAJONZI YATAWALA WAKATI WA KUMUAGA BIBI MAGDALENA PETRO MAGIGE

 Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Magdalena Petro Magige likiteremshwa kutoka kwenye gari tayari kwa kutoa heshima ya mwisho kabla ya safari ya kwenda kuupumzisha kijiji cha Kamange,Tarime mkani Mara.

 Ndugu , Jamaa na marafiki waliojitokeza kuja kutoa heshima za mwisho kwa mpendwa wao Bibi Magdalena Petro Magige aliyefariki  tarehe 19 Aprili jijini Dar es Salaam.
 Padri Valence Matungwa akitoa somo wakati wa misa maalum ya kumuaga marehemu Magdalena Petro Magige,Mikocheni jijini Dar es Salaam.
 Padri Ladislaus Kapinga akiongiza ibada wakati wa kumuaga marehemu Magdalena Petro Magige
 Mtoto wa Marehemu Norah P. Mukami akipokea ekaristi takatifu wakati wa misa maalumu ya kumuaga Magdalena Petro Mukami.
 Ndugu na jamaa waliojitokeza kwa wingi kwenye kutoa heshima ya mwisho kwa marehemu Magdalena Petro Magige.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza jambo na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Alhaji Adam Kimbisa naMkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) mstaafu, Jenerali George MwitaWaitara wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Magdalena Petro Magige.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Magdalena Petro Magige kilichotokea tarehe 19 Aprili 2015, jijini Dar es salaam.
  Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) mstaafu, Jenerali George MwitaWaitara akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Magdalena Petro Magige.
 Mzee Galius Abeid akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Magdalena Petro Magige.
 Ndugu na Jamaawakitoa heshima za mwisho
 Ilikuwa ni majonzi kwa kila mtu wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa Bibi Magdalena Petro Magige.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa heshima ya mwisho kwa Bibi Magdalena Petro sanjali na Mama Norah P. Mukami.
 Watoto wa marehemu Magdalena Petro Magige wakitoa heshima za mwisho kwa mama yao mpendwa aliyefariki tarehe 19 Aprili 2015.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akifunga jeneza la marehemu Magdalena Petro Magige.

No comments: