Posted by
Vempin Media Tanzania
on
- Get link
- X
- Other Apps
MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Rashidi Makwilo maarufu kama ‘Chid Benz’, aliyekuwa anatuhumiwa kwa kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin na bangi, leo ameachiliwa huru kwa kulipa faini ya Sh. 900,000.
Katika maelezo ya awali yaliyosomwa na mwendesha mashtaki wa Jamhuri Diana Lukendo, mbele ya Hakimu Warialwande Lema, msanii huyo alimwambia hakimu kuwa mshtakiwa alikamatwa na dawa hizo za kulevya akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, akitaka kusafiri kuelekea mkoani Mbeya.
Hata hivyo mshtakiwa huyo ambaye alikiri kosa mnamo tarehe 18 Aprili mwaka huu, leo aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu na kwamba asingetumia tena ulevi huo na atawaelimisha vijana wenzake juu ya madhara yake.
(NA GABRIEL NG’OSHA NA LAURENT SAMATTA/GPL)
Comments