Thursday, February 26, 2015

KAMPUNI YA SIMU YA OBI MOBILES YADHAMIRIA KUSAMBAZA TEKNOLOJIA KWA WATU WENGI NCHINI TANZANIA

unnamed
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Obi Mobiles, Bw Amit Rupchandani (kati kati) wakionyesha simu mpya aina ya Obi Mobiles kwenye uzinduzi rasmi wa simu hizo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Farouk Jivani kutoka kampuni ya Direct Specialist na Kushoto ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Obi Mobiles, Yusuf Kamal Khan .
………………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
 Mwanzilishi wa Obi Mobiles na Mkurugenzi Mtendaji wa zamani Apple, John Sculley aahidi utendaji wenye tija katika vifaa vya simu za mkononi chini ya nembo ya Obi nchini.
Kampuni ya Obi Mobiles inalenga kuongeza mauzo kupitia mpango mkakati unaowalenga vijana na walaji wengine 
kupitia aina mbalimbali ya simu ambayo itakuza upatikanaji wa mtandao na kufanya Tanzania moja ya nchi bora katika upatikanaji wa teknolojia ya mawasiliano.
Tanzania: Februari 24, 2015 – Obi Mobiles, Simu yenye teknolojia mpya na nembo ya Mwanzilishi na Mkongwe katika mambo ya Masoko na Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Apple, John Sculley, ni mbia mpya katika kampuni ya Inflexionpoint yenye makao makuu Sculley’s Toronto, Nembo hii mpya ya kampuni ilifanya uzinduzi wake mkubwa nchini India na Mashariki ya Kati mwaka 2014. 
Walengwa wakubwa katika kampuni hii ni vijana na watu wanaokwenda na wakati wa matumizi ya simu za mkononi, Simu na vifaa vya Obi vimepokelewa kwa hamasa kubwa katika masoko na simu ina matumaini wataendelea kupata wateja wengi siku za usoni.
Kampuni ya Obi Mobiles ilizindua aina saba za simu mbalimbali kwa ajili ya soko la Tanzania. Aina hizo za simu ni kama vile Hornbill S551 kwa TSh 350,000, Falcon S451 TSh 290,000, Crane S550 TSh 270,000, Wolverine S501 TSh220,000, Fox S453 TSh160,000, Racoon S401 TSh 130,000 na Power GO F240 – simu yenye uwezo mkubwa na vipengele mbalimbali 2,800mAH betri, na ina Power Bank (chaji benki) yenye uwezo wa kuchaji simu nyingine TSh 50,000.
Imani ya msingi katika kampuni ya Obi Mobiles ni kwamba teknolojia ni kitu cha lazima kwa kila mtu na uunganishwaji ni fursa ya kufungua mianya ya nafasi za biashara na kusaidia kukua kiuchumi na maendeleo ya kijami.
kwa taifa husika. Maono ya John Sculley ni kuhakikisha kwamba teknolojia isiwe kikwazo kwa mtu yeyote kupata kutokana na matatizo ya kimtandao au vikwazo vyovyote ambavyo vitasababisha watu wengi zaidi kukosa fursa hii.
Smartphones mpya za Android zilizozinduliwa na Obi Mobiles hutoa huduma bora zaidi na teknolojia ya hali ya juu na kwa mantiki hiyo kutoa fursa kwa watumiaji wa Tanzania kuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kufurahi intaneti kupitia uzinduzi wa simu hizo saba tofauti tofauti, uzinduzi rasmi wa simu hii kutoka kampuni ya Obi ni Mwezi Machi tarehe 7.
Akizungumza juu ya mkakati wa kampuni hiyo Afrika, Mkurugenzi Mtendaji wa Obi Mobiles MENA, Amit Rupchandani, alisema: “Wateja wanaongezeka kwa kuangalia jinsi ya kuboresha matumizi ya simu zao za mkononi kutoka katika simu za zamani kwenda kwenye simu za (smartphones). Hata hivyo, gharama kubwa za uwekezaji katika vifaa ya simu hizi mpya- na umri wa simu hizi mpya na matamanio ya wanunuzi wapya ni wakati mwafaka kwa kampuni ya Obi Mobiles, ambao tunaamini kutia alama ya vema katika box hili jipya katika maswala ya ubora wa simu, bei ili kuweza kuwafikia kila aina ya mteja katika soko ili kuongeza thamani katika soko la simu bara la Afrika,”

No comments: