


Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnuye akikutana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alipofika katika Ofisi za Free Media, wachapishaji wa gazeti la Tanzania Daima, akiwa katika ziara katika vyombo vya habari ambayo aliianza jana, jijini Dar es Salaam.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana kwa furaha na Mhariri Mtendaji wa Free Media, Nevile Meena alipowasili kwenye kampuni hiyo akiwa katika ziara kwenye vyombo vya habari mjini Dar es Salaam

Nape akizungumza na baadhi ya viongozi wa kampuni ya Free Media wachapishaji wa gazeti la Tanzania Daima jijini Dar es Salaam

Nape akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Ofisi za gazeti la Jambo Leo, jijini Dar es Salaam, akiwa katika ziara hiyo. Wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concept inayochapisha gazeti hilo, Theophil Makunga.

Nape akiwa katika mazungumzo na uongozi wa kampuni ya Jambo Concept

Nape akifafanua jambo wakati wa mazungumzo hayo na uongozi wa Jambo Concept

Nape akimuonyesha Makunga Kalenda ya CCM ya mwaka huu (2015) kabla ya kumkabidhi kama zawadi.

Nape akimkabidhi zawadi ya kalenda ya CCM, Makunga

Baadhi ya waandishi wa habari katika chumba cha habari cha magazeti ya Jambo Leo

Nape akiwa kwenye chumba cha Breaking news cha magazeti ya Jambo Leo

Nape akiagana na mpigapicha mkuu wa Jambo Leo Richard Mwaikenda mwishoni mwa ziara katika chumba cha habari cha magazeti hayo. Picha na Bashir Nkoromo na Adam Mzee
No comments:
Post a Comment