Friday, February 20, 2015

AIRTEL YAMTANGAZA BINGWA WA AIRTEL TRACE MUSIC, YAMZAWADIA MILIONI 50TZS

 Meneja Masoko wa Airtel Aneth Muga (kushoto) akimkabidhi
mshindi wa Airtel Trace Music Stars Nalimi Mayunga hundi ya mfano
yenye dhamani ya sh. 50mil baada ya kuibuka mshindi wa mashindano ya
Airtel Trace Music Stars, pia atapata fursa ya kwenda kuiwakilisha
nchi yetu katika mashindano ya Airtel Trace Stars ya Afrika
yatakayofanyika Mjini Nairobi Kenya mwezi machi,  anaeshuhudia ni
Afisa Uhusiano na matukio  wa Airtel Dangio Kaniki.

  Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Nalimi Mayunga akifurahia
zawadi yake baada ya kuibuka mshindi wa mashindano hayo yaliyofanyika
hivi karibuni. Mshindi huyo pia atapata fursa ya kwenda kuiwakilisha
Tanzania katika mashindano ya Airtel Trace Stars ya Afrika
yatakayofanyika Mjini Nairobi Kenya mwezi machi,

Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Nalimi Mayunga (kati)
akiwaimbia waandishi wa Habari (hawapo pichani) katika hafla ya
makabidhiano  ya zawadi yake hundi ya sh. Milioni 50 kushoto yake ni
Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki (kushoto)  na Meneja
Masoko wa Airtel Aneth Muga (kulia).


 ============   ======  ===========
Airtel yamtangaza Bingwa wa Airtel Trace Music, yamzawadia milioni 50TZS
*       Nyota wa Airtel Trace Music Stars apatikana
Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel leo imemtangaza rasmi mshindi wa
shindano la Airtel Trace Music star, shindano lilidumu kwa muda wa
miezi mitatu maalum kwa wasanii chipukizi kuweza  kuimba na kutuma
nyimbo zao kwa kutumia simu zao za mkononi kama studio kwa  lengo la
kusaka na kuibua vipaji kwa wanamuziki chipukizi nchini.

Akiongea na waandishi wa habari Meneja Masoko wa Airtel Aneth Muga
alisema"Leo tunayofuraha kubwa kumtangaza mshindi wetu wa shindano la
Airtel Trace Music Stars mara baada ya kuchaguliwa na majaji na
kupigiwa kura na watanzania.

"Washiriki watano ni kati ya wengi waliothubutu kuonyesha uwezo wao wa
kushiriki kwa kupiga simu, kuimba na kutuma nyimbo zao na hatimae
majaji wamesikiliza vipaji vyao kama walivyoimba na kuwachagua kuingia
tano bora (top 5)" alifafanua Muga.

Washiriki waliokuwa wamebahatika kuingia tano bora ni   Nalimi Mayunga
  mwenye namba ya ushiriki (55100182), Christopher Kihwele (5510050),
Tracy Eminence (55100420), Beautus Henry (55100106) na Rose Mbuya
(55100366).

Mshindi wetu ni Nalimi Mayunga mwenye namba ya ushiriki (55100182)
ambae amechaguliwa na majaji wetu pamoja na kupigiwa kura nyingi na
wananchi.

Zawadi yake ni milioni Tshs 50mil, na pia atapata fursa ya kwenda
kuiwakilisha nchi yetu katika mashindano ya Airtel Trace Stars ya
Afrika  Nairobi Kenya  yanayoshirikisha nchi 13 barani Afrika ambapo
pia mshindi atakaepatikana atarekodiwa nyimbo zake katika studio za
kimataifa nchini uingereza, na kupewa  mafunzo toka kwa msanii nguli
wa Afrika Akon.

Nchi nyingine zinazoshiriki mashindano haya na zitakazotoa jumla ya
vijana  13 barani Afrika ni pamoja na Kenya, Uganda Zambia,
Madagascar, Malawi, Nigeria, Ghana, Burkina Faso, Chad, Congo
Brazzaville, The Democratic Republic of Congo (DRC), na Gabon

No comments: