Kamati ya Bunge ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi yafanya ziara ya kikazi Jijini Dubai

 Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira na Mbunge wa Kahama, James Lembeli akiwa na Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai, Omari Mjenga katika picha ya pamoja
 Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira na Mbunge wa Kahama, James Lembeli akiwa na Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai, Omari Mjenga katika picha ya pamoja
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akiwa na Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai, Omari Mjenga na Mbunge wa Viti Maalum, Ester Bulaya katika picha ya pamoja, Dubai
 Wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira wakiwa Dubai na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi


Kamati ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. James Lembeli, imetembelea Manispaa ya Dubai na Mji wa Michezo wa Dubai (Dubai Sports City).

Aidha, Mhe. William Lukuvi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliongozana na Kamati. Ziara hii fupi imekuwa ya mafanikio makubwa, kwani kamati pamoja wajumbe wengine wamekubaliana masuala muhimu ambayo wameona yanafaa kuishauri Serikali kuyafanyia kazi ili kuwa na Mipango Miji ya kisasa.

Mhe. Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai aliongozana na ujumbe huu wa Kamati wakati wote wa ziara.

Comments