Friday, February 13, 2015

NAPE NNAUYE AITAKA TUME KUJIBU HOJA KWA WAKATI

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva akisalimia na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwenye mkutano wa pamoja na viongozi wa vyama vya siasa wa kujadili maboresho ya uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa, Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuvaakisalimiana na Katibu wa NEC Organaizeshen CCM,Dk.Mohamed Seif Khatibu
Wadau mbali mbali wa vyama vya siasa
Mwenyekiti
wa Chama cha United Demoratic (UDP), John Cheyo akipitia ratiba wakati wa mkutano huo
 Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva (kushoto),
akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja na viongozi wa vyama vya siasa wa
kujadili maboresho ya uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na Kura
ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa, Dar es Salaam
 Mwenyekiti
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (kushoto), akiteta na Katibu Mkuu wa ACT -Tanzania,
Samson Mwigamba wakati wa mapumziko. Viongozi hao waliwahi tibuana na
kusababisha Mwigamba kuhamia chama hicho kipya kutoka Chadema

 Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (kushoto) akizungumza jambo na
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia (kulia) pamoja na Katibu Mkuu wa
Chadema, Willbrod Slaa wakati wa mapumziko katika mkutano wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi na Viongozi wa vyama vya siasa wa kujadili maboresho ya uandikishaji
wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa,
Dar es Salaam
 Msajiri
wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa Tume ya Uchaguzi na wadau wa Vyama Vya Siasa.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza wakati wa mkutano huo ambapo aliwaambia Tume ya Uchaguzi inabidi iwe na utaratibu wa kujibu maswali ama hoja za wananchi kwa wakati ili kuondoa wasiwasi wa kuelewa.
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akichangia hoja kwenye mkutano huo.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye (kulia) akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Chadema Dk.Wilbrod Slaa.

No comments: