MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA SHULE YA SEKONDARI ANGAZA HUKO LINDI MANISPAA NA MATAWI YA CCM KATIKA KATA YA WAILES

 1
Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), anayewakilisha Lindi Mjini, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Shule ya Sekondari Angaza Ndugu Upendo Muro mara baada ya kuwasili shuleni hapo tarehe 12.2.2015. Mama Salma alitembelea shuleni hapo kuona maendeleo ya shule hiyo pamoja na kusalimiana na walimu na wanafunzi.
2
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM Mama Salma Kikwete akiwasalimia walimu wa Shule ya Sekondari ya Angaza iliyopo Manispaa ya Lindi Mjini tarehe 12.2.2015.
16
14
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) anayewakilisha Lindi Mjini na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi wa Kata ya Wailes kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Tawi la Angaza tarehe 12.2.2015.
3
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) anayewakilisha Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akipanda mti katika eneo la Shule ya Sekondari ya Angaza ikiwa ni kumbukumbu ya kutembelea shule hiyo tarehe 12.2.2015.
6
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Angaza wakati alipotembelea shule hiyo tarehe 12.2.2015.
10 
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM, Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa Shule ya Sekondari Angaza iliyoko Lindi Manispaa mara baada ya kuitembelea na kuzungumza na walimu pamoja na wanafunzi wa shule hiyo tarehe 12.2.2015.
PICHA NA JOHN  LUKUWI.

Comments