Ziara ya Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa Kilimanjaro na Arusha

 Mwenyekiti wa Bodi ya NHC, Mhe. Zakia Meghji alipotembelea eneo ambalo jengo la biashara la ghorofa litakalojengwa Moshi Mjini mkoa wa Kilimanjaro plot no 97/Block I Aga Khan Rd/Market Str. Kushoto ni Bw. Juma Kiaramba - Kaimu Meneja, mkoa wa Kilimanjaro, Bi. Susan Omari - Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii na Bw. Fred Steven - Kitengo cha Matengenezo, Mkoa wa Kilimanjaro
 
Mwenyekiti wa Bodi ya NHC, Mhe. Zakia Meghji akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro kwenye ziara ya kutembelea shughuli za Shirika.
 Kiongozi wa kikundi cha Faraja Youth Community Group cha Halmashauri ya Siha akisoma risala kwa mgeni rasmi Mhe. Zakia Meghji alipowatembelea kuona shughuli za kikundi hicho. Kushoto kwake ni Afisa Vijana wa Halmashauri ya Siha Bw. Anselim Hamaro.
 Mwenyekiti wa Bodi ya NHC, Mhe. Zakia Meghji na Kaimu Meneja, mkoa wa Kilimanjaro wakifurahia jambo baada ya kutembelea Hotel ya Camel iliyofanyiwa matengenezo hivi karibuni, Plot 7H Mawenzi, Double Road. 
 Mwenyekiti wa Bodi ya NHC, Mhe. Zakia Meghji na Bi. Susan Omari wakipata maelezo ya mradi wa Satellite City wa Mateves, Arusha kutoka kwa Bw. James Kisarika, Meneja mkoa wa Arusha.
 Mwenyekiti wa Bodi ya NHC, Mhe. Zakia Meghji na Bi. Susan Omari wakipata maelezo ya mradi wa Safari City eneo la Mateves, Arusha kutoka kwa Bw. James Kisarika, Meneja mkoa wa Arusha
 
 Mwanakikundi cha Faraja Youth Community Group alitoa maelezo ya jinsi ya kufyatua matofali mbele ya Mwenyekiti wa Bodi ya NHC, Mhe. Zakia Meghji.
 
Mwenyekiti wa Bodi ya NHC, Mhe. Zakia Meghji akizungumza na baadhi ya vijana wa kikundi cha Faraja Youth Community Group.
 
 Kaimu Meneja Bw. Juma Kiaramba na Afisa Matengenezo Bw. Fred Steven wa mkoa wa Kilimanjaro wakitoa maelezo ya ujenzi unaondelea ili kukamilisha  nyumba ya makazi ya meneja wa mkoa kiwanja namba 21K Karanga.
 Mwenyekiti wa Bodi ya NHC, Mhe. Zakia Meghji akisaini kitabu cha wageni alipotembelea kikundi cha vijana Faraja Youth Community Group. Kulia kwake ni  Bi. Susan Omari - Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii na Bw. Juma Kiaramba - Kaimu Meneja, mkoa wa Kilimanjaro.
Mwenyekiti wa Bodi ya NHC, Mhe. Zakia Meghji na Bi. Susan Omari wakipata maelezo ya mradi wa Usa River Satellite City, Arusha kutoka kwa Bw. James Kisarika, Meneja mkoa wa Arusha 

Comments