Monday, February 23, 2015

YANGA YAICHAPA MBEYA CITY 3-1

MRISHO-NGASSA

VINARA wa Ligi Kuu Vodacom, Yanga, jana huko Sokoine, Jijini Mbeya wamepaa kileleni wakiwa Pointi 5 mbele ya Timu ya Pili na Mabingwa Watetezi, Azam FC, baada ya kuichapa Mbeya City Bao 3-1.
Bao za Yanga hii Leo zilifungwa na Simon Msuva, Mrisho Ngassa na Amisi Tambwe wakati lile la Mbeya City lilipachikwa na Peter Mapunda.
Katika Mechi nyingine ya Ligi iliyochezwa Leo huko Kambarage, Stand United waliitungua Simba Bao 1-0.
Mechi ya mwisho hii Leo itachezwa Usiku huu huko Azam Complex, Chamazi, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam kati ya Azam FC na Tanzania Prisons.

No comments:

RAIS SAMIA ASHIRIKI NA KUTUNUKU TUZO ZA WASANII WA KOMEDI TANZANIA 2025

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameshiriki kama mgeni rasmi katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Wasa...