Pichani juu na chini ni , ni Mhe. Mjenga akimkaribisha Mhe. Janeth Mbene ofisini kwake kwa mazungumzo
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Janeth Mbene yupo ziarani Dubai. Katika ziara hiyo, Mhe. Mbene ameutembelea Ubalozi Mdogo wa Tanzania uliopo Dubai na kufanya mazungumzo na Mhe. Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Tanzania. Aidha, Mhe. Mbene amepata maelezo ya kina kuhusu shughuli za Ubalozi Mdogo na Kituo cha Biashara.Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara Ndugu Ruhumbika, amemueleza Mhe. Mbene ni kwa jinsi gani Ubalozi Mdogo kwa kushirikiana na Kituo hicho wameweza kuvutia wawekezaji wengi kwenda Tanzania.
Kwa upande wake, Mhe. Mjenga amemuomba Mhe. Mbene kuwa Serikali iangalie uwezekano wa kujenga ofisi zake za Ubalozi Mdogo ambazo zitakuwa na nafasi kubwa kwa ajili ya maonyesho ya bidhaa za Tanzania kwa muda wa mwaka mzima. Nchi nyingi zilizo na Ubalozi Mdogo na Kituo cha Biashara hapa Dubai, wameweza kuvutia uwekezaji na uuzaji wa bidhaa za biashara zinazotoka kwenye nchi zao kwa utaratibu huu.
Comments