JAHAZI NA MASHAUZI KUTIFUANA USIKU WA BABA NA MWANA

jaha1
Usiku wa Baba na Mwana
Hatimaye makundi mawili yanayoaminika kuwa na mashabiki wengi zaidi katika taarab, Jahazi Modern Taarab na Mashauzi Classic yatafanya onyesho la pamoja mwezi ujao.
Onyesho hilo litafanyika Travertine Hotel Magomeni jijini Dar es Salaam, Jumapili ya tarehe 22 mwezi Machi.
Hii inakuwa ni mara ya pili kwa makundi hayo mawili kufanya onyesho la pamoja (bila kushirikishwa makundi mengine).
Onyesho la kwanza lililopewa jina la Usiku wa Baba na Mwana lilifanyika miaka minne iliyopita ndani ya ukumbi huo huo na inaaminika kuwa hadi leo bado rekodi yake ya mahudhurio pale Travertine haijavunjwa.
Mzee Yussuf na Isha Mashauzi ambao ni wamiliki wa makundi hayo, wameiambia Saluti5 kuwa onyesho hilo ni “Usiku wa Baba na Mwana …Season 2”.
Viongozi hao wamesema onyesho hilo ni la kukuza udugu pamoja na kuwakutanisha pamoja mashabiki wao na kamwe halina hata chembe ya wala mpambano.

Comments