WAZIRI CHIKAWE AWAPA SOMO MAKATIBU KATA CCM NACHINGWEA, MKOANI LINDI
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto) akizungumza na Makatibu Kata wa CCM, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi. Katika mazungumzo hayo yaliyojumuisha Makatibu Kata zaidi ya 30, Waziri Chikawe aliwataka viongozi hao kuhakikisha wanazunguka katika kata zao kuhakikisha wanawahamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwa ajili ya maandalizi ya kuipigia kura Katiba inayopendekezwa pamoja na Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika mwaka huu nchini. Katikati Meza Kuu ni Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Mussa Liliyo akifuatiwa na Mwenyekiti wa Makatibu Kata hao, Ally Napepa.
No comments:
Post a Comment