Monday, February 16, 2015

MAANDALIZI SENSA YA VIWANDA YAKAMILIKA, SERIKALI YAWATAKA WADAU KUTOA USHIRIKIANO.

1
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa  akifunga rasmi mafunzo ya siku 14 ya wasimamizi na wadadisi wa Sensa ya viwanda 2013 itakayofanyika nchini nzima kuanzia Februari 23,2015. Hafla ya kufunga mafunzo hayo ilifanyika jana eneo la  Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika jijini Dar es salaam.

2

Makamu Mkuu wa chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Dkt. Tumaini Katunzi akizungumza na wasimamizi na wadadisi wa Sensa ya Viwanda itakayofanyika nchi nzima kuanzia Februari 23 mwaka huu jana jijini Dar es salaam wakati wa kufunga mafunzo ya wadadisi hao.

3

Baadhi ya wadadisi wa Sensa ya Viwanda wakifuatilia hafla ya ufungaji wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kukusanya takwimu za Sensa ya Viwanda ya mwaka 2013 iliyofanyika jana katika Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika eneo la Changanyikeni jijini Dar es salaam.

4

Kamishna wa Viapo ambaye pia ni Mwanasheria wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Oscar Mangula akitoa ufafanuzi kwa wasimamizi na wadadisi wa Sensa ya Viwanda (hawapo pichani) kuhusu  Sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia Sensa ya Viwanda ya mwaka 2013 inayotarajia kufanyika nchi nzima kuanzia Februari 23, 2015.

5

Baadhi ya wadadisi wa Sensa ya Viwanda wakisaini fomu za viapo vyao mbele ya Kamishna wa Viapo Bw. Oscar Mangula (hayupo pichani) jana jijini Dar es salaam mara baada ya kuhitimu mafunzo  ukusanyaji wa takwimu  za Sensa ya Viwanda 2013 itakayofanyika Februari 23 mwaka huu.

6

Wadadisi wa Sensa ya Viwanda 2013 wakiapa mbele ya Kamishna wa Viapo  Bw. Oscar Mangula (hayupo pichani) jana jijini Dar es salaam mara baada ya kuhitimu mafunzo ya siku 14 ya kuwajengea uwezo wa ukusanyaji wa takwimu  za Sensa ya Viwanda 2013 itakayofanyika nchi nzima kuanzia Februari 23 mwaka huu

No comments: