Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF Mzee Emannuel Humba akionyesha tuzo yake aliyopewa na mfuko huo kwa kutambua mchango wake akiwa mwanzilishi wa mfuko huo wakati wa hafla ya kuwaaga viongozi na wafanyakazi wastaafu iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee mwishoni mwa wiki , Mzee Emannuel Humba aliwaasa wafanyakazi wa mfuko huo kushikamana na kufanya kazi kwa kujituma ili kuhakikisha mfuko huo unafikia malengo, Katika hafla hiyo Emanuel Humba pia amezawadiwa zawadi mbalimbali. wa pili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF Balozi Ali Mchumo na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo Bw. Michael Mhando.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE)Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF akitoa shukurani zake kwa uongozi wa NHIF na wafanyakazi kwa ujumla kwa kuwaadalia hafla hiyo ya kuwaaga.Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF akipokea shada la maua kutoka kwa Balozi Ali Mchumo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF.Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti akizungumza katika hafla hiyo wakati akielezea wasifu wa baadhi viongozi wastaafu wa mfuko huo.Dr Marqus Kalinga Mstaafu wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa akipokea tuzo yake kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF Balozi Ali Mchumo, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Michael MhandoAthman Rehani Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) akisoma wasifu wa mmoja wa wastaafu.Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF Balozi Ali Mchumo akikabidhi zawadi kwa mstaafu Andrew Mwilungu aliyekuwa meneja wa NHIF Pwani.Mstaafu Peter Daniel akitoa shukurani zake mara baada ya kukabidhiwa zawadi zake katika hafla hiyo ya kuwaaga wastaafu wa Mfuko wa Bima Afya ya Taifa, kutoka kushoto wanaofurahia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Michael MhandoBaadhi ya wafanyakazi wakijadili jambo wakati wa hafla hiyo.Wafanyakazi wakiwa na nyuso za furahaKaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Michael Mhando akizunguma katika hafla hiyo.Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Michael Mhando kushoto akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Balozi Ali Mchumo kulia na Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen MikongotiMkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti, Othman Rehani Mkurugenzi wa Afya ya Jamii CHF na Mkurugenzi wa Tiba na Masuala ya Kiufundi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dk.Frank Lekey wakipitia makabrasha wakati wa hafla hiyo.Balozi Ali Mchumo Akisalimiana na Mkurugenzi Mstaafu wa NHIF Bw. Emannuel Humba.Balozi Ali Mchumo Mwenyekiti wa Bodi Akiwasili ukumbini hapo huku akiwa ameongozana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu Bw. Michael Mhando.Baadhi ya wafanyakazi wakimpokea mwenyekiti wa Bodi.Hapa wakiserebuka kidogoWafanayakzi wakiwa wamejipanga huku wakifurahia jambo wakati wa mapokezi ya viongozi na wafanyakazi wastaafu wakati walipowasili kwenye ukumbi wa Diamond tayari kwa hafla hiyoMzee Emanuel Humba pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wakiinga ukumbini hapo huku wakipokelewa na wafanyakazi.Baadhi ya maofisa Grace Michael kushoto Hawa Katikati na Catherin wakipozi kwa pichaWafanyakazi hao wakimpelekea keki Kaimu Mkurugenzi mkuu NHIF Bw. Michael Mhando.Balozi Ali Mchumo Mwenyekiti wa Bodi akimpongeza Kaimu Mkurugenzi Mkuu Bw. Michael Mhando pamoja na baadhi ya wafanyakazi.Kutoka kushoto Maofisa wa NHIF Sabina Komba na Luhende Singu wakiwaongoza maofisa wenzao kufungua Shampeni wakati wa hafla hiyo.
Comments