TAARIFA KWA UMMA

index
Mfuko wa Pensheni wa PSPF unawatangazia kwamba 
Mkutano Mkuu wa Nne wa wadau wake utafanyika tarehe 
18 na 19 Februari 2015 kuanzia saa mbili na nusu 
asubuhi hadi saa kumi na moja jioni katika Ukumbi wa 
Mikutano wa hoteli ya St. Gasper – Dodoma. 
Madhumuni ya Mkutano huu ni kutoa taarifa ya mwaka 
ya Mfuko, kutathmini maendeleo na changamoto 
zinazoukabili Mfuko na Sekta ya Hifadhi ya Jamii nchini. 
Kauli mbiu ya mkutano huu ni; 
“PSPF – CHAGUO LAKO SAHIHI” 
Tafadhali thibitisha ushiriki wako kwa Mkurugenzi Mkuu, 
Dar es Salaam au ofisi za PSPF mikoani. 
Imetolewa na 
Mkurugenzi Mkuu, PSPF. 
MFUKO WA PENSHENI WA PSPF 
PSPF Tanzania @PSPF Tanzania www.pspf-tz.org 0800 110 055 / 0800 780 060

Comments