Thursday, February 19, 2015

VIJANA WILAYANI KASULU WAPEWA SOMO KUHUSU FURSA ZA MFUKO WA MAENDELEO YA VIJANA

kas1Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mhe. Dani Makanga (watatu kutoka kulia kabla ya mabadiliko) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo walipomtembelea ofisini kwake leo. Kutoka kulia ni Afisa Utamaduni na Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Bw. Mbogo, Afisa Vijana kutoka Wizara ya
kas2Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mhe. Dani Makanga akizungumza na wajumbe kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo waliofika ofsini kwake kwa ajili ya kujitambulisha kabla ya kuendelea na ratiba yao ya mafunzo kwa Vijana wa Halmashauri za Kasulu na Bihigwe leo mjini Kasulu. Katikati ni Mkuu wa msafara huo ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa na wa kwanza kushoto ni Afisa Vijana wa wizara hiyo Bi. Amina Sanga.kas3Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Bw. Bernard Ntikabuze (kushoto) akiagana na akipeana mkono na Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga wakati walipotembelea ofisini kwa Mkurugenzi huyo leo. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa.kas4Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu Bw. Muguha Titus Muguha akizungumza na Vijana wanaoshiriki mafunzo kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (hawapo pichani) yanayotolewa na wataalamu kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Kutoka kulia ni Afisa Vijana wa Wizara hiyo Bi. Amina Sanga, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria Bibi. Esther Riwa, Mkuu wa Kituo cha Maendeleo ya Vijana Sasanda kilichopo Mbeya Bw. Laurian Massele na Afisa Vijana wa Mkoa wa Kigoma Bw. Edward Manase
kas5Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa akitoa mada kuhusu Sera ya Maendeleo ya Vijana na Stadi za Maisha kwa baadhi ya Vijana wa Halmashauri za Kasulu na Buhigwe leo katika Ukumbi wa Kituo cha Utamaduni Wilayani Kasulu.
kas6Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa akitoa mada kuhusu Sera ya Maendeleo ya Vijana na Stadi za Maisha kwa baadhi ya Vijana wa Halmashauri za Kasulu na Buhigwe leo katika Ukumbi wa Kituo cha Utamaduni Wilayani Kasulu.
kas7Baadhi ya Vijana wakifuatilia mada zilizokuwa zilizokuwa zikiwasilishwa na Mkuu Mkuu wa Kitengo cha Sheria Kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa haypo pichana leo mjini Kasulu.kas8Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga akitoa maada kuhusu Mwongozo wa Mkopo wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo Wilayani Kasulu wakati wa mafunzo kwa Vijana wa Halmashauri za Kasulu na Buhigwe.Jumla ya Vijana 66 wamehudhuria mafunzo hayo.
kas9Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Bw. Bernard Ntikabuze akizungumza na ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo walipofika ofisini kwake ili kujitambulisha kabla ya kuendelea na ratiba ya mafunzo na ukaguzi wa miradi Wilayani hapo leo.

No comments: