Friday, November 14, 2014

WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII AFUNGUA KONGAMANO LA NHIF NA WAANDISHI WA HABARI MJINI DODOMA

1Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mh. Dr. Seif Rashid akifungua Kongamano la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na wahariri pamoja na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali linalofanyika kwenye hoteli ya New Dodoma  mkoani Dodoma jana, Kongamano hilo la siku mbili linaendelea leo na linajadili mafanikio mbalimbali na changamoto zinazokabili mfuko huo katika mikoa mbalimbali na Halmashauri ambazo unatoa huduma zake. Kongamano hilo linamalizika leo(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DODOMA)2Naibu Katibu wa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dr. Deo Mtasiwa  akizungumza katika kongamano hilo wakati akimkaribisha waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Seif Rashid ili kuzungumza na washiriki wa kongamano hilo.3Kamimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Khamis Mdee  akitoa maelezo kuhusu shughuli mbalimbali kwa mwaka mzima.4Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa masoko na Utafiti NHIF,Raphael MwamotoKaimu Mkurugenzi Tiba na Ushauri wa NHIF, Dk Mkwabi Fikirini na Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii CHF Athman Rehani wakiwa katika mkutano huo.5Hance John Mwankenja Afisa Mwandamizi , Matekelezo NHIF pamoja na maafisa wengine wa mfuko huo wakiwa katika kongamano hilo.006Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mh. Elibariki Kingu akitoa mada katika kongamano hilo.6Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii CHF Bw. Athman Rehani akitoa mada katika Kongamano hilo.7Mkuu wa Wilaya ya Igunga na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Fatma Said Ally wakiwa katika kongamano hilo.9Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari wakifuatilia mada mbalimbali katika kongamano hilo.10Grace Kingalame wa TBC wa pili na wadau wengine wakiwa katika kongamano hilo.11Hosea Cheyo wa TBC Mbeya kushoto na Tom Chilala wa Star TV wakifuatilia mada.12Wanahabari mbalimbali wakifuatilia kongamano hilo.131415Baadhi ya maofisa wa NHIF wakiandika mambo muhimu katika kongamano hilo.

No comments: