Mwili wa Marehemu Hamis Kayumbu Amigolas akiwekwa kwenye gari mara baada ya kutolewa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya taifa ya Muhimbili jana tayari kwa mazishi ambayo yalifanyika jana arlasiri kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam ambapo wanamuziki , ndugu jamaa na marafiki mbalimbali pamoja na waombolezaji wengine walijitokeza kwa ajili ya kumzika marehemu Amigolas ambaye aliwahi kutamba na bendi ya African Stars Twanga Peteta kabla ya kweda Ruvu Stars Band ya JKT. Waumini wa Dini ya Kiislamu, wakiusalia mwli wa aliyekuwa mwanamuziki wa Ruvu Stars Band na Twamga Pepeta huko Mburahati Kinondoni jijini Dar es salaam kabla ya kwenda kumzika.Waombolezaji wakiubeba mwili wa marehemu Hamis Kiumbu AmigolasWasani mbalimbali wakijadiliana jambo katika makaburi ya Kisutu baada ya kuuhifadhi mwili wa marehemu Hamis Kiumbu Amigolas.Waombolezaji wakisawazisha kaburi la aliyekuwa mwana muziki wa Twanga Pepeta katika makaburi ya Kisutu Baadhi ya Waombolezaji wakiwa wanauweka mwili wa marehemu Hamis Kayumbu ‘Amigolas’, Aliyekuwa Mwanamuziki wa bendi ya Ruvu Stars Band na African Stars Twanga Pepeta Dar es Salaam jana katika Makaburi ya Kisutu.(PICHA NA KHAMISI MUSSA)
Comments