Wednesday, November 19, 2014

MOTO WATETEZA SOKO LA BIDHAA ZA UTAMADUNI LIJULIKANALO KAMA MT.MERU CURIOS & CRAFTS MARKET JIJINI ARUSHA




Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo ameagiza uchunguzi wa kina kufanyika kufuatia soko la wafanyabiashara wa Vinyago na bidhaa mbalimbali za kitalii la Maasai Market kuteketea kwa moto.
Mulongo ambaye alifatana na kamati ya Ulinzi na Usalama alishangaa kuona maduka hayo ambayo yapo jirani na Kikosi cha Zima Moto kushindwa kuzima moto na kusababisha hasara kwa wananchi.
"Sitakubali kuona uzembe unaendelea katika mkoa wetu,lazima watu wawajibishwe kwa uzembe hasa Kikosi cha kuzima moto ambao mko karibu na Ofisi za Chama Cha mapinduzi wilaya yalipo maduka haya"amesema Mulongo
Chanzo cha moto bado hakijaweza kufahamika huku maduka hayo yapatayo 188, huku yakiwa hayajaunganishwa na Umeme kwa lengo la kuepusha hatari ya moto kwani bidhaa nyingi ni vinyago vinavyotengenezwa kwa mbao.
Habari picha kwa hisani ya woindeshizza blog

Baadhi ya bidhaa zilizoteketea kwa moto katika SOKO la bidhaa za utamaduni lijulikanalo kwa jina la MT.MERU CURIOS& CRAFTS MARKET usiku wa kuamkia  jana. 








Sehemu ya Wafanyabiashara wa SOKO la bidhaa za utamaduni lijulikanalo kwa jina la MT.MERU CURIOS & CRAFTS MARKET wakiwa wameduwaa bila kujua la kufanya mara baada ya Soko hilo kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo na kuunguza bidhaa zote za wafanya biashara zililopo katika soko hilo.

No comments:

DKT. ABBASI AKAGUA MIRADI YA UTALII PORI LA AKIBA LA PANDE, ATOA MAAGIZO YA KUKAMILIKA KABLA YA AFCON 2027

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, leo Julai 23, 2026, ametembelea Pori la Akiba la Pande jijini Dar es Salaa...