Kituo cha Kisasa cha Uchunguzi na Matibabu ya magonjwa ya binadamu kinachojengwa katika Chuo Kikuuu cha Dodoma UDOMT kikiwa katika hatua za mwisho mwisho za ukamilishwaji, Kituo hiki kitahudumia wagonjwa kutoka maeneo mbalimbali ya mikoa ya jirani ya na mkoa wa Dodoma na kinajengwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF kwa gharama ya shilingi Bilioni 36 ambazo zimetolewa na mfuko huo kwa silimia 100, Akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali wanaohudhuria kongamano la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya linalofanyika kwenye hoteli ya Dodoma mjini humo walipotembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho, Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Mlacha Shaaban amesema “Kituo hiki kitajikita zaidi kwenye magonjwa ya uchunguzi na utafiti pia kitatoa wataalamu kutoka katika kitivo cha afya cha Chuo kikuu cha UDOM na wataalamu watakaofanya kazi katika kituo hicho watakuwa wakiffundisha wanafunzi na kuhudumia katika kituo hicho,Kituo hicho kinatarajiwa kuanza kutoa huduma ifikapo Januari 2015(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DODOMA)
Baadhi ya waandishi wa habari wakiingia katika jengo la kituo cha Utafiti na tiba cha UDOM kinachojengwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF.
Kaimu Makamu Mkuu wa chuo Kikuu cha UDOM Profesa Mlacha Shaaban akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali walipotembelea ujenzi wa kituo cha Tiba na Utafiti kinachojengwa katika chuo kikuu cha UDOM.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Raphael Mwamotoakizungumza na waandishi wa habari kwenye kituo hicho
Waandishi wa habari wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Raphael Mwamotoakimsikiliza Athman Rehani Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii CHF
Mshauri Mtaalam wa Mradi huo wa ujenzi wa kituo kutoka kampuni ya Hab Consult Bwana Habib Nuru akiwatembeza waandishi wa habari katika jengo hilo.
Mshauri Mtaalam wa Mradi huo wa ujenzi wa kituo kutoka kampuni ya Hab Consult Bwana Habib Nuru akitoa maelezo kwa waandishi wa habari wakati walipokuwa wakitembelea kituo hicho kulia kwake niMkurugenzi wa Masoko na Utafiti kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Raphael Mwamoto
Mganga Mkuu wa mkoa wa Singida Dr. Doroth Gwajima akitoa mada katika kongamano hilo linalofanyika mjini Dodoma kwa siku mbili.
Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari na waandishi wa habari wakiwa katika kongamano hilo.
Mwanaamani Mtoa Katibu wa Mkuu wa mkoa wa Tanga akiwaonyesha kitu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Galawa kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Taifa ya Afya NHIF Khamis Mdee.
Grace Michael mmoja wa maafisa wa NHIF akifuatilia jambo wakati mkutano huo ukiendelea.
Baadhi ya waandishi wakiwa katika mkutano huo.
Meneja wa Masoko wa NHIF Angela Mziray akisikiliza jambo wakati alipokuwa akiongea na Grace Mchaele mmoja wa maofisa wa mfuko huo.
Comments