Thursday, November 13, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KWENYE MAZISHI YA RAIS SATA WA ZAMBIA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata Ikulu mjini Lusaka Zambia juzi Novemba 11,2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal wa kwanza (kushoto) akiwa na Rais Mstaafu wa Zambia Mhe. Rupia Banda, Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta, Rais wa Msumbiji Mhe. Ermando Guebuza na Kaimu Rais wa Zambia Dkt. Guy Scott kwenye Misa Maalum ya kuaga mwili wa Rais Michael Sata iliyofanyika juzi Novemba 11,2014 kwenye Uwanja wa Taifa mjini Lusaka Zambia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama cha Tawala cha PF Mhe. A.B. Chikwanda kwenye Viwanja vya Ubalozini katika Makaburi ya Viongozi wa Kitaifa wakati mazishi ya Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata yaliyofanyika juzi Novemba 11,2014 kwenye uwanja wa Taifa mjini Lusaka Zambia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimfariji Rais mstaafu wa kwanza Zambia Dkt. Keneth Kaunda mara baada ya kumalizika maziko ya Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata kwenye Viwanja vya Ubalozini katika Makaburi ya Viongozi wa Kitaifa yaliyofanyika juzi Novemba 11,2014 mjini Lusaka Zambia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimfariji Rais mstaafu wa Zambia Mhe. Ruphia Banda baada ya kumalizika mazishi ya Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata kwenye Viwanja vya Ubalozini katika Makaburi ya Viongozi wa Kitaifa yaliyofanyika juzi Novemba 11,2014. katikati Rais mstaafu wa kwanza wa Zambia Dkt. Keneth Kaunda. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisaini kitabu cha maombolezo ya Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata kwenye Viwanja vya Ubalozini katika Makaburi ya Viongozi wa Kitaifa yaliyofanyika juzi Novemba 11,2014. (Picha na OMR)

No comments: