Katibu Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo (kulia) akieleza jambo wakati wa mkutano wa kujadili mambo yanayohusu tasnia ya filamu Tanzania uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa wa Bodi hiyo, Bw. Benson Mkenda.
Wadau kutoka Bodi ya Filamu Tanzania pamoja na Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) wakimsikiliza Katibu wa TAFF (hayupo pichani) wakati alipokuwa akichangia mada kuhusu masuala ya filamu nchini wakati wa mkutano uliofanyika katika Ofisi za Bodi ya Filamu jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO-DSM)
Comments