Wednesday, November 05, 2014

WATANZANIA WATAKIWA KUDUMISHA AMANI NA MSHIKAMANO

unnamed
Aliyekuwa MJumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Amon Mpanju ambaye pia ni mwenyekiti wa wa shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es salaam kuhusu umuhimu wa Vijana kuwa wazalendo na kulinda amani iliyopo hapa nchini kwa maslahi mapana ya Taifa.
unnamed2
Aliyekuwa MJumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Amon Mpanju ambaye pia ni Mwenyekiti wa wa Shirikisho la vyama vya Watu wenye ulemavu Tanzania akitoa wito kwa Watanzania kusoma na kuelewa Katiba inayopendekezwa ili kuepuka upotoshaji unaofanywa na watu wachache kwa maslahi yao.
………………………………………………………………………….
Frank Mvungi-Maelezo
Watanzania wametakiwa kuendeleza amani na mashikamano uliopo kwa maslahi ya Kizazi hiki na Kizazi Kijacho kwa kuenzi misingi ya Amani na Uzalendo iliyojengwa na Waasisi wa Taifa hili.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na aliyekuwa MJumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Amon Mpanju ambaye pia ni mwenyekiti wa wa shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania.¬
Nchi ni zaidi ya itikadi na Mihemko ya watu wachache hivyo ni lazima tuwaepuke wote wanaotaka kuvuruga amani na utulivu uliopo

alisema Mpanju
Akifafanua Mpanju amesema hali iliyojitokeza katika moja ya midahalo iliyofanyika jijini Dar es salaam hivi karibuni ni ya kukemewa na watu wote wanaopenda amani na wazalendo kwa kuwa vitendo hivyo vinaweza kuleta madahara katika jamii hasa kwa makundi maalum kama walemavu,wanawake na wataoto.
Akizungumzia Katiba inayopendekezwa Mpanju amesema ni vyema Watanzania wakaisoma na kuilewa ili kuepuka upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu kwa maslahi yao binafsi.
Aliongeza kuwa ni vyema kuepuka kauli zinazoweza kuleta uchochezi katika jamii hasa katika kipindi hichi ambapo baadhi ya watu wamekuwawakitumia mwavuli wa Kutoa elimu kwa wananchi kuhusu Katiba inayopendekezwa na kufanya vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani.
Pia Mpanju alitoa wito kwa vijana kuwa mstari wa mbele katika kupinga vitendo vyote vinavyoweza kupelekea uvunjifu wa amani hapa nchini kwa kuweka uzalendo mbele na kujali maslahi mapana ya Taifa na si ya Kikundi Fulani cha watu.
Katika Hatua nyingine Mpanju alikanisha kuhusika na vurugu zilizotokea katika moja ya midahalo hapa jijini Dar es salaam na kudai hahusiki na tukio hilo kwa namna yoyote kama ilivyoripotiwa .

No comments: