TASWIRA KUTOKA BUNGENI BAADA YA KIKAO KUAHIRISHWA LEO ASUBUHI

Mwenyekiti wa Bunge, Mh. Mussa Azan Zungu akiongozwa na Mpambe wa Bunge kutoka kwenye ukumbi wa Bunge wakati alipositisha kikao cha Bunge cha asubuhi leo na kuahidi kujibu miongozo yote katika kikao cha jioni huku akisema bunge halijapokea barua yoyote kwa mjadala wa Escrow kukatazwa kujadiliwa bungeni.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki na Mbunge wa Urambo, Mh. Samuel Sitta (katikati) akizungumza na baadhi ya wabunge wa Upinzani, Bungeni mjini Dodoma leo Novemba 26, 2014.
Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda akizugumza na Mbunge wa Viti Maalum Rachel Mashishanga kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma leo Novemba 26, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Comments