KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YAFANYA ZIARA YA KUKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA BARABARA YA BAGAMOYO – MAKOFIA – MSATA (KM 64) PAMOJA NA MIZANI YA KISASA ILIYOPO ENEO LA VIGWAZA


Naibu waziri wa Ujenzi Mhe. Gerson Lwenge (Mb) akiwasili eneo la mradi akiambatana na Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Peter Serukamba.
Wajumbe wa kamati ya bunge ya Miundombinu wakipata taarifa ya mradi wa ujenzi wa barabara ya lami Bagamoyo – Makofia – Msata (Km 64) kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Patrick Mfugale.
Ramani ya mchoro ambao barabara ya Bagamoyo – Makofia – Msata itaungana na barabara ya Dar es salaam – Bagamoyo.
Mkandarasi Kampuni ya Estim Construction Ltd,akiendelea na kazi ya ujenzi wa barabara hiyo.
Daraja la kioga lililopo kwenye barabara ya Bagamoyo – Makofia – Msata lenye urefu wa meta 55 limekamilika ujenzi wake.
Mhe. Gerson Lwenge naibu Waziri wa ujenzi aliyenyoosha mkono akitoa maelezo ya ujenzi wa daraja kubwa la mto Ruvu chini lenye urefu wa meta 140 kwa wajumbe wa kamati ya Miundombinu.
Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Miundombinu wakionekana kwa mbali wakishuhudia mtambo wa kuchimba mashimo kwa ajili ya ujenzi wa nguzo za daraja ukifanya kazi eneo la mto Ruvu chini daraja hili litakuwa na urefu wa meta 140.
Naibu waziri wa Ujenzi Mhe. Gerson Lwenge pamoja na wajumbe wa kamati ya Miundombinu wakiangalia eneo la mto Ruvu chini ambapo daraja litapita.
Msafara wa wajumbe wa kamati ukikagua barabara hiyo huku wakielekea mizani ya kisasa eneo la Vigwaza.
Wajumbe wa kamati ya Miundombinu wakipewa taarifa walipowasili eneo la mizani, Vigwaza.
Picha ya mizani ya Vigwaza ikionekana kwa mbali huku magari makubwa na madogo yakipishana.
Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Patrick Mfugale akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa mizani ya kisasa eneo la Vigwaza wa wajumbe wa kamati ya Miundombinu.

Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Miundombinu wamefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Bagamoyo – Makofia – Msata (km 64), inayojengwa kwa kiwango cha lami. Barabara hii inaunganika na barabara kuu ya Dar es salaa – Chalinze – Arusha katika eneo la Msata. Hivyo ni njia mbadala ya kutoka Dar es Salaam kwenda mikoa ya kanda ya Kaskazini na nchi jirani ya Kenya.

Barabara hii inayojengwa na kampuni ya Estim Construction ltd, na kusimamiwa na mhandisi mshauri kampuni ya JBG Gauff Ingenieure GMBH & Co. Mkandarasi wa barabara hii ya Bagamoyo – Makofia – Msata anatarajia kukabidhi barabara hii Machi, 2016.

Aidha, kamati hiyo ilipata nafasi ya kutembelea mizani ya kisasa iliyopo eneo la Vigwaza inayojengwa na kampuni ya M/S China Henan International Cooperation Group Co. Ltd (CHICO) na mhandisi mshauri kampuni ya Ambicon Engineering Ltd of Tanzania. 

Mradi huu hadi sasa umekamilika kwa asilimia 95. Ikiwa ni kukamilika kwa barabara ya maingilio, maegesho ya magari, majengo, ofisi, gereji na jenereta, vyoo vya wasafiri pamoja na mizani. 

Mradi huu unakamilika Novemba 2014. Kwa habari zaidi tazama picha za ziara hiyo.(Imetolewa na kitengo cha mawasiliano serikalini – Wizara ya Ujenzi)

Comments