Wednesday, November 19, 2014

JENGO LA KIHISTORIA LAPOROMOKA HUKO ZANZIBAR‏

Jengo moja la gorofa laporomoka huko Zanzibar katika eneo la kihistoria Jaws Corner ndani ya manispaa ya mji mkongwe Zanzibar.
Taarifa zinasema wananchi wa karibu na eneo hilo wakishirikiana na vikosi maalumu vya serikali vinaendelea kufanya jitihada mbali mbali katika eneo hilo ikiwemo kuhakikisha hakuna athari zaidi zitakazoweza kutokea.
Baadhi ya shuhuda mmoja ameiambia mazrui media kuwa watu wana wasiwasi juu ya uwepo wa watu wawili waliokua wakipita njia hawana uhakika kama waliwahi kuvuka au laa.
Hadi sasa juhudi za kuondoa kifusi cha jengo hilo kimeanza ili kuweza kubaini kama kuna watu wowote wale waliojeruhiwa au kupoteza maisha.

No comments:

RAIS SAMIA ASHIRIKI NA KUTUNUKU TUZO ZA WASANII WA KOMEDI TANZANIA 2025

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameshiriki kama mgeni rasmi katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Wasa...