VITUKO VYATAWALA MAZISHI YA MSANII MABOVU IRINGA , MLEVI AFANYA VURUGU KUBWA


Wasanii  wakielezea kifo cha mabovu , Juu ni Msanii Mabovu enzi za uhai  wake

Waombolezaji  wakiwa na jeneza la msanii Mabovu kutoka msikiti wa Mwangata kwenda makaburi ya Mlolo Iringa
Wasanii wakiwa  wamelipiga chata kaburi la mabovu mara baada ya mazishi yake
Baadhi ya  wasanii wa kundi la Weusi ambao  wamefika  Iringa kumzika msanii Mabovu leo
Makini akichangisha rambi rambi
Msanii JOh Makini akiwa na michango ya msiba wa mwenzao Mabovu leo
Mwakilishi  wa  wasanii wa kundi la Weusi Joh Makini kushoto  akimpa pore baba wa msanii Mabovu mzee Upete kulia baada ya kumaliza kuzika nyumbani kwake Mwangata wengine ni baadhi ya  wasanii  walioshiriki mazishi hayo leo
Mwakilishi wa kundi la weusi kwanza Joh Makini akizungumza na mtandao huu wa matukiodaima leo
Picha na habari na kikosi cha matukiodaima.co.tz 
Vituko vyatawala msiba wa msanii Ahmed Zubery Upete a. k. a Geez Mabovu Iringa mlevi (pichani aliyekaa chini)atembeza kichapo kwa wafiwa kisa ataka aruhusiwe kuufukua mwili wa marehemu ili auage Mara ya mwisho asisitiza kuwa marehemu amekua nae na ana siri nzito ya kifo chake.
Tukio hilo limetokea muda mfupi baada ya mwili wa marehemu kuwasili makaburi ya Mlolo nje kidogo ya mji wa Iringa kwa mazishi.
Chapombe huyo ambae alifika makaburini hapo kwa kuchelewa alivamia eneo hilo la mazishi kwa kuanza kutoa lugha za matusi ya nguoni kwa wafiwa kwa madai wamewezaje kumzika marehemu huyo bila ya yeye kufika eneo hilo.
Kutokana na lugha hizo za matusi iliwalazimu Vijana waombolezaji kumtoa kwa nguvu eneo hilo na kwenda nae pembeni kidogo kumsihi asifanye vurugu kabla ya chapombe huyo kuanza kurusha Ngumi kwa wasanii.
Akizungumza  mara  baada ya mazishi hayo  mmoja  kati ya  wadau  wa  tasinia ya muziki nchini na promota mkubwa wa mziki nyanda za  juu  kusini Edwin Bashir ambae ni  mtangazaji  wa  kituo cha  Radio Ebony  Fm alisema  kuwa  mbali ya umoja ambao  wasanii  wameuonyesha katika msiba huo kwa  kuja kushiriki mazishi  ila bado angeshauri  wasanii kwa  wakati mwingine  kujenga ushirikiano wa  kumjulia hali mwenzao pindi anapoumwa.
” Sisemi  kwa  ubaya  ila kiukweli  msanii  Geez Mabovu  ameumwa sana karibu mwaka mzima anasumbuliwa na ugonjwa  wake ila hakuna  msanii ambae amefika  kumjulia hali  ila  leo wengi  wamesafiri  kuja kumzika….. inapendeza  kusaidiana  wakati wa ugonjwa badala ya  kusubiri mwenzenu afe “
Bashir  alisema  kuwa msanii  huyo ni  miongoni mwa  wasanii  wa mwanzo zaidi  kuutangaza mkoa wa Iriga katika tasnia ya  muziki na kuwa hata kabla ya vituo vya radio  kuanzishwa mkoani Iringa alikuwa akiutangaza mkoa na kusikika katika  radio  mbali mbali za nje ya Iringa.
Alisema  kuwa msanii  huyo toka amemaliza  elimu  yake kamwe  hajapata kufanya  shughuli  nyingine  nje ya mziki na kuwa  wakati  wote  alikuwa akijishughulisha na muziki  zaidi .
Hata  hivyo  alisema chanzo cha Mabovu kuhama mkoa wa Iringa na kuhamishia makazi yake  jijini Dar es Salaam ni  kuzidi  kuutangaza muziki  zaidi na mkoa wake wa Iringa malengo ambayo alipata  kufanikiwa kwa  kiasi  kikubwa .
” Utaona   jinsi ambavyo  msiba  wake  leo  ulivyowavuta  watu  wegi  wapenzi na wadau wa muziki  kutoka mikoa mbali mbali ya nje ya Iringa ambao kimsingi  baadhi yao  imekuwa ni mara yao ya kwanza kufika Iringa ….pamoja na kufarijika kwa  umati wa  watu  waliofika kumzika  ila  moyo umeniuma sana hasa  ukizingatia kuwa   kifo  chake hakikuwa na  ghafla bali  amekufa kwa mateso makubwa kwa  kuugua  karibu mwaka  mzima  sasa hivyo kwa  umoja  huo ningetegemea wangefika enzi za uhai  wake kumuuguza mwenzao”
Kwa  upande wake mwakilishi  kwa  kundi   la Weusi Bw  Joh Makini alisema  kuwa  kifo cha Mabovu  kimeacha  pengo kubwa katika tasnia  ya  muziki hasa muziki wa hiphop Tanzania,
 Alisema  kuwa  Mabovu  amepata  kuishinae Kinondoni  Jijini Dar es Salaam  mtaa mmoja  ila  pia amepata  kushirikiana  kazi mbali mbali  za kimzuki .
Hivyo  alisema  kuwa  ushirikiano  huo  ndio  ambao umewasukuma  kufika mkoani Iringa  kushiriki mazishi  hayo baada ya  pengo kubwa ambalo  wamelipata .
Akizungumza  kwa niaba ya  wasanii wazawa na mkoa wa Iringa msanii Squza,alisema  kuwa  Iringa  imempoteza  msanii mkongwe na  kuwa kifo  chake  kitaenziwa na  wasanii wa mkoa wa Iringa  pia  ambao  wapo nje ya mkoa huo kwa kuangalia jambo la kufanya  katika kuwanyanyua  wasanii chipukizi wa mkoa huo.
Alisema  kuwa  wapo  wasanii maarufu  wengi  kutoka mkoa wa Iringa ambao  wana majina makubwa kama  Rehema Chalamila (RAY C} akina  MiKe T  na  wengine  wengi na kuwa  kama  njia ya  kumuenzi  Mabovu  watahakikisha wanaunganisha  nguvu kwa kushirikiana na vyombo  vya habari  kuona Iringa inampata mwakilishi mwingine wa Mabovu kutoka kwa  wasanii Chipukizi .
Msanii Mabovu  alifariki  dunia jana  majira ya saa 2 usiku  nyumbani kwa wazazi  wake eneo la Mwangata mjini Iringa ambako alikuwa akiugulia na amezikwa  leo katika makaburi ya Mlolo nje  kidogo na mji wa Iringa

Comments