Mfungaji wa bao pekee la Simba dhidi ya Ruvu Shooting, Emmanuel Okwi akishangilia wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Taifa. (Picha na Francis Dande wa Blogu ya Jamii)
Wachezaji wa Simba wakishangilia baada ya Okwi kuifungia timu yake bao pekee.
Wachezaji wa Simba wakishangilia baada ya Okwi kuifungia timu yake bao pekee.
Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi akiwatoka mabeki wa Ruvu Shooting.
Elius Maguli akiwatoka mabeki wa Ruvu Shooting.
Mchezaji wa Ruvu Shooting, Abdulrahman Musa (kulia) akiwania mpira na Elius Maguli wa Simba.
Kocha wa Simba, Patrick Phiri akikumbatiana na Okwi baada ya mchezo na tmu yake kupata ushindi wa kwanza tangu kuanza kwa Ligi.
Makipa wa Simba, Peter Manyika JR na Steven Mapunda (kulia) wakishangilia ushindi wa kwanza wa Simba tangu kuanza kwa Ligi Kuu.
Wachezaji wa Simba wakishangilia ushindi wa timu yao baada ya kuifunga Ruvu Shooting 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Okwi akishangilia baada ya kumalizika mpira.
Okwi akiwa na furaha baada ya kuifungia timu yake bao pekee.
Mashabiki wa Simba wakiwa na furahi.
Comments