Majembe ya Skylight Band yakiporomosha burudani kwa mashabiki wake Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar. Kutoka kushoto ni mkongwe kwenye muziki wa dansi Joniko Flower a.k.a Baba lao, Sony Masamba a.k.a Fally Ipupa wa Bongo na Sam Mapenzi.
Pichani juu na chini ni mashabiki nao wakijibu mapigo ya sebene lililokuwa likiporomoshwa na majembe ya Skylight Band.
Kutoka kushoto ni mkongwe kwenye muziki wa dansi Joniko Flower a.k.a Baba lao, Sony Masamba a.k.a Fally Ipupa wa Bongo na Sam Mapenzi wakiwapa raha mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
Usishangae kumuona Sony Masamba kavua shati na kubaki na vest..ilikuwa ni patashika na nguo kuchanika…Joniko Flower akisongesha burudani.
SAM MAPENZI…..Kuna watu hatari, wenye mapenzi zenye siri kali…Letu nalo lina jua kali, penzi letu serikali…Wajua nakupenda, malaika…….ANETH KUSHABA AK47:……Kuna wengi walafi, fimbo zao haziui mbali…Wengi wao wajidai, mimi kwako no, sitawai…Mmm take me, nitembee nawe….Baby take me, nitembee nawe… bonge moja la kolabo njoo ulishuhudie mwenyewe kwa macho yako.
Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 akifanya yake jukwaani kuhakikisha mashabiki wake wanapata furaha na tabasamu nyusoni mwao, usikose usiku wa leo ndani ya Thai Village kuanzia saa tatu usiku.
Mashabiki wa Skylight Band wakijinoma na muziki mzuri kwa kujinafasi ndani ya kiota cha Thai Village Ijumaa iliyopita.
If I should stay…..I would only be in your way…..So I’ll go but I know…I’ll think of you every step of the way…..And I… will always love you, ooh….Will always love you…You….My darling, you…….Mmm-mm…si mwingine ni Bela Kombo katika hisia kali za kuteka mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita ndani ya Thai Village, tukutane baadae kwa play list kali na nyimbo kali zilizoenda shule.
Bela Kombo akiimba na zawadi ya ua kutoka kwa shabiki aliyekunwa na wimbo huo.
Hashim Donode akifanya yake huku akipewa sapoti na mwanadada Bela Kombo.
Rappa Joniko Flower akiporomosha mistari huku waimbaji wenzake wakisebeneka jukwaani.
Mashabiki nao walicharukaje sasa…..palikuwa hapatoshi uwanjani.
Comments