BENKI YA UWEKEZAJI YA ULAYA (E.I.B), YAIPIGA JEKI BENKI YA CRDB

Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima akiwasili ukumbini wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba wa mkopo wa sh. Bilioni 43 kutoka Benki ya Uwekezaji Ulaya. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi CRDB, Martin Mmari na (katikati) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei na kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa.
Mwakilishi wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya, Nikolaos
Milianitis (kulia) akisaini mkataba wa mkopo wa sh. bilioni 43 na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB,
Dk. Charles Kimei baada ya Benki hiyo kwa ajili ya kuwakopesha wafanyabiashara Wadogo na Wakati. Hafla hiyo
ilifanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Wa pili kushoto anayeshuhudia ni Naibu Waziri wa
Fedha, Adam Malima. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari na Wa pili kulia ni, Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya, Eric Beaume.
Mwakilishi wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya, Nikolaos
Milianitis (kulia) akibadilishana hati na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB,
Dk. Charles Kimei baada ya benki hiyo kusaini mkopo wa billion 43 na benki ya
CRDB kwa ajili ya kuwakopesha wafanyabiashara Wadogo na Wakati. Hafla hiyo
ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Katikati anayeshuhudia ni Naibu Waziri wa
Fedha, Adam Malima. 
Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki
ya CRDB, Tully Mwambapa (wa pili kushoto), Meneja Mahusiano wa Benki
ya
 CRDBGodwin Semunyu (wa pili kulia)
wakiwa katika hafla ya uwekaji saini wa mkataba wa mkpo wa sh. bilioni 43 na
Benki ya Uwekezaji Ulaya.
Maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja.
Milianitis (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya, Eric Beaume (kulia) akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya, Nikolaos Milianitis (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto) na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB pamoja na wadau wengine.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji saini mkataba wa mkopo wa sh. bilioni 43 kutoka Benki ya Uwekezaji Ulaya.
Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza katika hafla hiyo.
Mwakilishi wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya, Nikolaos Milianitis akizungumza katika hafla hiyo.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.
Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima (kushoto) akiwa na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya, Eric Beaume.  
Meza Kuu.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka akifuatilia kwa makini hafla ya uwekaji saini wa mkataba wa mkopo wa sh. Bilioni 43 na Benki ya Uwekezaji Ulaya.
Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB, Martin Mmari akizungumza katika hafla hiyo.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima akitoa hotuba yake wakati wa hafla hiyo.
…………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
BENKI ya CRDB imesaini mkataba wa mkopo wa sh. bilioni
43 baina ya benki ya uwekezaji Ulaya (E.I.B)
kwa ajili ya kuwakopesha na kuwasaidia wafanyabiashara wanaofanya shughuli za
kukuza uchumi.
 
Akizungumza jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki Mkurugenzi Mtendaji
wa CRDB, Dk. Charles Kimei alisema benki yake kwa kushirikiana na EIB imeamuwa
kusaidia jamii nchini hivyo mkataba huo ni mwanzo wa ushirikiano endelevu
utakaohamasisha upatikanaji wa ajira.
 
Alisema kufanyakazi na benki ya EIB kutasaidia kukuza
biashara katika maeneo muhimu kama uvuvi, usindikaji wa chakula, usafiri,
biashara pamoja na huduma zote za kiuchumi.
 
“Mimi kama kiongozi wa CRDB Tanzania ninamamlaka ya
kusaidia hizi sehemu za soko na kuongeza jitihada za kumaliza umaskini, pia
kuongeza shughuli za kiuchumi za wateja wetu ili kufikia lengo la kuongeza
mapato katika benki yetu,” alisema Kimei.
 Kwa upande wake Naibu
Waziri wa Fedha Adam Malima alisema mkataba huo pia una lengo la kuisaidia
benki ya CRDB katika kuendesha shughuli zake mbalimbali.
 
Alisema ni jambo la faraja kuona benki kama EIB imekubali
kuiamini CRDB na kuipa mkopo wa kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya kuwasaidia wafanyabiashara.
“Tunachokiamini kuwa hii benki kutoka Ulaya siyo benki
ndogo ni kati ya benki kubwa zilizopo hapa duniani, sasa kama wamekuja hapa
kwetu na wakaonyesha nia njema ya kutusaidia endapo watabaini kuwa pesa zao azitatumika
kwa malengo yaliyokusudiwa watavunjika moyo,” alisema.

Comments