Mkurugenzi Mtendaji wa Skylight Band Dkt. Sebastian Ndege a.k.a JembeniJembe akizungumza na wakazi wa Mwanza kuwakaribisha kwenye show ya SKYMOTO iliyofanyika kwenye hekalu la maraha la Jembe Beach lililopo Malimbe jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Skylight Band Dkt. Sebastian Ndege a.k.a JembeniJembe akimtambulisha Mkurugenzi wa Yamoto Band Said Fella almaarufu kama Mkubwa na wanawe kwa wakazi wa jijini Mwanza waliotinga kwenye hekalu la maraha lililo Malimbe jijini Mwanza Jembe Beach.
Vijana wa Skylight Band ndani ya Jembe Beach jijini Mwanza wakifungua burudani kwa kumpa sapoti Digna Mbepera (wa pili kulia) kutoa burudani kwa wakazi na mashabiki wa Skylight Band mwishoni mwa juma. Kutoka kushoto ni Sony Masamba, Aneth Kushaba AK47 pamoja na Hashim Donode (kulia).
Divas wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 na Digna Mbepera wakionyesha ufundi wao ndani ya Jembe Beach.
Rapa mkongwe wa muziki wa dansi Joniko Flower (kushoto) akiongoza kikosi cha Skylight Band kutoa burudani kwa wakazi wa jijini Mwanza kwenye show ya aina yake iliyopewa jina la SKYMOTO huku wakikolabo na Yamoto Band ndani ya Jembe Beach jijini Mwanza.
Raia wa kigeni na couple yake wakiburudika na burudani kutoka vijana wa Skylight Band ndani ya Jembe Beach jijini Mwanza.
Sam Mapenzi wa Skylight Band akiwa raha wakazi wa jijini Mwanza ndani ya Jembe Beach mwishoni mwa juma walipo kolabo na Yamoto Band.
Aneth Kushaba AK47 akiwa chezesha ligwaride wakazi wa Mwanza ndani ya Jembe Beach.
Comments