WAZIRI MUHONGO AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA MCC

8
9Makamu wa Rais wa Mfuko wa Changamoto za Millenia (MCC) Kamran Khan ( wa kwanza kushoto ) akimweleza jambo Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (wa kwanza kulia) anayesikiliza katikati ni Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress mara baada ya kikao hicho.
11Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospter Muhongo katikati) katika picha ya pamoja ofisini kwake na Makamu wa Rais wa Mfuko wa Changamoto za Millenia (MCC) Kamran Khan (kushoto) na Balozi wa Marekani nchini , Mark Childress (Kulia)..
……………………………………………………………………
Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amekutana na Makamu wa Rais wa Mfuko wa Changamoto za Millenia (MCC) Kamran Khan na Ujumbe wake akiwemo Balozi wa Marekani nchini Mark Childress, katika kikao kilicholenga kujadili maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa MCC Awamu ya pili na masuala ya kuendeleza sekta ya nishati nchini. 
Kikao hicho kimezihusisha pia taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini ikiwemo, Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) pamoja na taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (EWURA). 
Katika kikao hicho, Profesa Sospeter Muhongo amezitaka taasisi hizo kutekeleza miradi hiyo kwa kasi zikizingatia suala la uwajibikaji, ubunifu, uwazi na kuongeza kuwa, miradi hiyo itatekelezwa bila kuwepo na mazingira ya rushwa , huku akisisitiza ushirikiano baina ya serikali na sekta binafsi katika uendelezaji wa miradi hiyo.
Kwa upande wake Makamu wa Rais wa MCC, Kamran Khan ameahidi kutoa ushirikiano kwa Wizara katika kutekeleza miradi hiyo ambayo inalenga kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na umeme wa uhakika na wa kutosha. 
Kwa upande wake Balozi wa Marekani nchini Mark Childress amesisitiza suala la kuzingatia muda katika utekelezaji wa miradi hiyo na kuongeza kuwa, hakuna sababu itakayokwamisha miradi hiyo.

Comments