
MMOJA wa wataalamu wa kuchunguza matatizo ya masikio, Stuart Specer kutoka Taasisi ya Starkey Hearing Foundation ya nchini Marekani inayoendesha kliniki ya masikio aakitaniana na mkazi wa Arusha, Ally Abdulrahman aliyewahi kuishi nchini humo ambaye kwa sasa ana matatizo ya kusikia kwenye kliniki inayofanyika kwenye viwanja vya Hoteli ya Kibo Palace Jijini Arusha jana
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mount Meru na chuo cha Biashara cha Arusha (IAA) waliokuja kujitolea wakisaidia kutoa huduma mbalimbali kwenye kliniki ya masikio iliyoratibiwa kwa pamoja kati ya Montage Limited na Starkey Hearing Foundation inayofanyika kwenye viwanja vya Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha
Wagonjwa wenyematatizo ya usikivu wakisubiri kupata matibabu kwenye kliniki ya matibabu na uwekaji vifaa vya kuongeza kiwango cha usikivu iliyoratibiwa kwa pamoja kati ya Montage Limited na Starkey Hearing Foundation inayofanyika kwenye viwanja vya Hoteli ya Kibo Palace.

DAKTARI, Assay Shibanda(kushoto) na John Yuccas wakimwekea mwanafunzi wa Shule ya Msingi Elbol,Levina Innocent mashine ya kuongeza kiwango cha usikivu kwenye Kliniki inayoendeshwa kwa pamojakati ya Montage Limited na taasisi kutoka Marekani ya Starkey Hearing Foundation ya kuwawekea vifaa vya kuongeza usikivu inayofanyika kwenye viwanja vya Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha


No comments:
Post a Comment