TRA yaendelea na Maadhimisho ya Wiki ya Mlipa Kodi Tanzania,Yatoa Msaada Hospitali ya Temeke na Kukabidhi Madawati 100 Shule ya Msingi Misitu,Kivule
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakijadiliana jambo wakati wakijiandaa kwenda kufanya usafi wa Mazingira wa Hospitali ya Temeke,Jijini Dar es Salaam jana Novemba 18,2014.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), jana Novemba 18,2014 walitembelea Hospitali ya Rufaa ya Temeke jijini Dar es Salaam,ambapo waliweza kutoa msaada wa vitu mbali mbali kwa watoto waliolazwa Hospitalini hapo pamoja na kukabidhi baadhi ya vifaa vya Usafi kwa Uongozi wa hospitali hiyo Mbali na kukabidhi vifaa hivyo,pia walijumuika pamoja na kujitolea kufanya usafi wa Mazingira ya Hospitali hiyo.
Mara baada ya kukamilisha shughuli zote za hospitalini hapo,Wafanyakazi hao walielekea moja kwa moja katika Shule ya Msingi Misitu,ilipo katika Kata ya Kivule,Kitunda na kuweza kukabidhi msaada wa Madawati 100 ambayo yatapunguza adha ya kukaa chini kwa asilimia 74 ya wanafunzi wote wa shule hiyo ambao idadi yake imefikia 590.
Hapo awali wanafunzi hao wote walikuwa wakikaa chini na kuendelea na masomo yao.
TRA imefikia kufanya hivyo,ikiwa katika muendelezo wa Maadhimisho ya Wiki ya Mlipa Kodi chenye kauli mbiu isemayo "Risiti ni Haki Yako,Unaponunu Dai Risiti na Unapouza ni Lazima Utoe Risiti" ambayo kilele chake ni Novemba 21,2014 huku Mgeni Rasmi akitazamiwa kuwa Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Bilal.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiendelea kufanya usafi wa Mazingira katika maeneo mbali mbali Hospitali ya Temeke,Jijini Dar es Salaam jana Novemba 18,2014.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Kanda ya Temeke,Victor Msuya (kulia) akizungumza na mmoja wa wauguzi wa zamu katika Wadi ya Watoto ya Hospitali ya Rufaa ya Temeke jijini Dar es Salaam jana Novemba 18,2014,wati Timu TRA ilipotembelea Wadi hiyo.
Baadhi ya Watoto waliolazwa kwenye Wadi hiyo.
Daktari akichukua vipimo kwa mmoja wa watoto waliolazwa kwenye Wadi ya Watoto ya Hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam huku mzazi wake akimuangalia.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Kanda ya Temeke,Victor Msuya (kulia) akiwaongoza maafisa wengine wa TRA kutoa bidhaa mbali mbali walizokwenda kuwagawia watoto wanaopatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Temeke,Jijini Dar es Salaam leo Novemba 18,2014.
Sehemu ya Maafisa wa TRA wakiwa nje ya jengo la Hospitali ya Temeka mara baada ya kumaliza kufanya usafi wa mazingira wa Hospitali hiyo.
Meneja wa Wagonjwa waliolazwa wa Hospitali ya Rufaa ya Temeke,Nuswe Ambokile akizungumza na wanahabari wakati akitoa shukrani kwa Uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuweza kujitoa kwao kwenda Hospitalini hapo na kutoa msaada waliofanikiwa kuutoa na kujitolea kwao kufanya usafi wa mazingira.
Picha ya pamoja.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Misitu,Ilipo katika kata ya Kivule,Kitunda jijini Dar es Salaam wakiwa wameketi kwenye madawati mapya yaliyokabidhiwa leo na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).Nyuma yao ni Baadhi ya Maofisa wa TRA waliofika shuleni hapo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Misitu,Hyasinta Hugo akizungumza wakati akiukaribisha Uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Shuleni hapo.
Mkurugenzi wa Walipakodi na Elimu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Richard Kayombo akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Tiagi Masamaki kuzungumza na uongozi wa Shule hiyo na kukabidhi madawati.
Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Tiagi Masamaki akizungumza na uongozi wa Shule hiyo pamoja na wanafunzi kabla ya kukabidhi madawati,yaliyotolewa na TRA kwa shule hiyo.
Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Tiagi Masamaki akizungumza na wanafunzi wa darasa la kwanza wa Shule ya Msingi Misitu.
Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Tiagi Masamaki akipena mkoni na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Misitu,Hyasinta Hugo wakati akimkabidhi madawati 100 yaliyotolewa na TRA kwa shule hiyo.
Diwani wa Kata ya Kivule,Mh. Nyasika Motewa akitoa shukrani zake za dhati kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa mchango wao huo kwa Shule ya Msingi Misitu iliopo kwenye Kata yake.
Sehemu ya wanafunzi wa Shule hiyo ya Misitu wamkisikiliza kwa makini Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Tiagi Masamaki.
Mmoja wa wanafunzi wa Shule hiyo akitoa Shukrani kwa niaba ya wanafunzi wenzake kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania.
Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa hapo awali,kabla TRA hawajapeleka madawati shuleni hapo.
Wanafunzi wakiendelea na masomo.
Comments