Mwanzilishi wa Taasisi ya Fazel, Dkt. Sajjad Fazel akisalimiana na Diwani wa Kigogo, Bw. Manyama wakati wa funguzi wa huduma ya upimaji wa afya bure kwa wakazi wa Kigogo. Katikati ni Imam wa Msikiti wa Al Ghadir, Sheikh Jalala.(Picha na habari naModewjiblog).
Kwa kuhakikisha jamii inakuwa katika hali ya usalama wa kiafya, Taasii ya Fazel Foundation kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu ya Afya na Madawa (TAHMEF) wametoa huduma ya upimaji wa magonjwa mbalimbali kwa wananchi wa Kigogo, Dar es Salaam.
Zoezi hilo lilifanyika Aprili, 23 katika Msikiti wa Al Ghadir uliopo Kigogo Post na jumla ya 352 wanawake wakiwa 150 na wanaumme 202 walipimwa Malaria, Kisukari, Shinikizo la Damu na Upungufu wa Damu mwilini.
Kati ya watu hao, watu 38 wameonekana kuwa na Shinikizo la Damu, 36 Upungufu wa Damu, 8 Kisukari na mmoja Maralia ambapo walipata nafasi ya kupatiwa dawa na ushauri kutoka kwa madaktari mbalimbali.
Aidha kwa mafanikio hayo, Fazel Foundation inawashukuru wote walioshiriki katika huduma hiyo akiwepo Dkt. Mohammed Alloo, Dkt. Sibtain Moledina, Mohammed Enterprises Tanzania Limited (METL Group), Salama Pharmaceuticals na Clinicheck Labs, Imam wa msikiti wa Al Ghadir Sheikh Jalala, Msikiti wa Al Ghadir, Diwani wa Kigogo, Bw. Manyama, Team ya Volunteers na Hawza ya Imam Sadiq kwa ushiriki wao katika zoezi hilo.
Comments