


……………………………………………………………………………………………………………KAMPUNI ya Ulinzi ya SGA imetoa msaada wa vifaa kusaidia waendesha bodaboda Mtaa Mbezi A, katika kujiepusha na ajali katika siku ya usalama duniani.
Akizungumza wakati wa kakabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Erick Sambu amesema kuwa vifaa walivyopewa vitasaidia katika kujiepusha na ajali kutokana na dereva wa gari kuona kifaa hicho.
Amesema kuwa vifaa hivyo vina thamani ya sh.milioni Nne na kuahidi kuendelea kutoa msaada katika makundi mbalimbali kutokana na kazi yao ya kuangalia usalama.
Sambu amesema kuwa SGA katika kuadhimisha siku ya usalama duniani na kuwataka wadau wengine kuunga mkono katika kuwangalia watu bodaboda.
Naye Mwakilishi wa Mwanyekiti wa Serikali ya Mtaa Mbezi A, Carolyne Ngoda amesema kuwa SGA wameokoa maisha ya vijana wao wanaoshughuli na biashara ya kusafirisa watu kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
No comments:
Post a Comment