Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Christina Lissu Mughwai, ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwenye Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam. Marehemu Christina Lissu Mughwai, alifikwa na umauti mwishoni mwa wiki iliyopita, kutokana na Maradhi ya Kansa yaliyokuwa yakimsumbua.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisaini kitabu cha Maombolezo ya Marehemu Christina Lissu Mughwai, ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwenye Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam.
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki ambaye ni Kaka wa Marehemu Christina Lissu Mughwai, Mh. Tundu Lissu, akisoma wasifu wa Marehemu, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wake, kwenye Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akimfariji Mtoto wa Christina Lissu Mughwai, mara baada ya kutoa taarifa ya Mama yake.
Comments