WAZIRI UMMY MWALIMU AADHIMISHA SIKU YA MALARIA DUNIANI KWA KUPIMA MALARIA KWA KUTUMIA MRDT

Ummy Mwalimu

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiwaonesha waandishi wa habari kipimo cha haraka cha kupima malaria(mRDT) wakati akitoa tamko la maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani leo kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha udhibiti wa Mbu waenezao Malaria Charles Dismas kutoka mpango wa Taifa wa kudhibiti Malaria.

Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amewataka watanzania kwa pamoja kuungana kupambana na ugonjwa wa Malaria ili kusaidiana na serikali kutokomeza ugonjwa huo ambao husababisha vifo vya watu wengi nchini.

Waziri Ummy ameyesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni siku ya Maralia Duniani ambapo huadhimishwa Aprili, 25 ya kila mwaka na kuwataka wananchi kushiriki kikamilifu ili kutokomeza ugonjwa huo.

“Msisitizo mkubwa wa Wizara yangu ni kwa wananchi na wadau wote kuona umuhimu na kutoa kipaumbele katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria kwa kuhakikisha matumizi sahihi ya mikakati iliyopo katika kuuthibiti ugonjwa huu,“Iwapo mikakati hiyo itatekelezwa ipasavyo ni dhahiri kuwa maambukizi yataendelea kupungua kwa kiasi kikubwa na hatimaye kumaliza kabisa tatizo hili,” alisema Waziri Ummy.
Waziri Ummy Mwalimu
Kaimu Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria, Dkt.Renata Mandike (kushoto) akitoa ufafanuzi kuhusiana na utekelezaji wa udhibiti wa Malaria nchini wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani). Kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu.
Malaria
Baadhi ya wataalam wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma pamoja na waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri Ummy Mwalimu.
mwalimu
Fundi sanifu maabara, Habiba Malima akimchukua damu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu kwa kipimo cha malaria Rapid Diagnosist Test(mRDT), kipimo hicho ni cha haraka na huchukua dakika ishirini kugundua kama una Malaria, kipimo hiki kilianza kutumika nchini mwaka 2009.
Richard Mwaikenda
Mwandishi wa habari na mmiliki wa globu ya mzee wa matukio, Richard Mwaikenda akichukuliwa kipimo cha malaria na fundi sanifu maabara Habiba Malima ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Malaria duniani katika ukumbi wa viwanja vya Bunge.

Comments