Waziri Mkuu wa mstaafu wa Kenya Raila Odinga akiwasili kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Chato Mkoani Geita kwa ajili ya kwenda kumsalimia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
...........................
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Raila Amoro Odinga amemtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyopo mapumzikoni katika Kijiji cha Kilimani, Wilaya ya Chato Mkoani Geita.
Mheshimiwa Odinga ambaye ameongozana na mkewe Mama Ida Odinga na Binti yake Winnie Raila Odinga, wametua kwa Helkopta katika uwanja wa Shule ya sekondari ya Chato leo tarehe 02 April, 2016 majira ya saa 11 jioni na baadaye kuelekea nyumbani kwa Rais Magufuli ambako wamepokelewa na wenyeji wao Rais Magufuli mwenyewe na Mkewe Mama Janeth Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga nyumbani kwake Chato mkoani Geita mara baada ya Kuwasili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikumbatiana na Waziri Mkuu wa mstaafu wa Kenya Raila Odinga mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Chato Mkoani Geita.
Akizungumza mara baada ya kuwasili Chato, Mheshimiwa Raila Odinga amesema yeye na familia yake wapo likizo na wamekuja kumtembelea rafiki wa familia yao, kwa lengo la kumsalimia.
"Nimekuja kupumzika na nimekuja na Mama na Mtoto wangu wa kike, na vilevile kuja kutoa pongezi kwa ndugu yangu kwani tangu achaguliwe sijakuja hapa Chato, na nilisema siendi Dar es salaam nitakuja hapahapa Chato" Alisema Mheshimiwa Odinga.
Pamoja na kukutana na Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Raila Odinga pia amemsalimu Mama wa Rais Bibi Suzana Joseph Magufuli na pia amezulu Makaburi walimozikwa wanafamilia wa Rais, akiwemo Baba Mzazi Mzee Joseph Magufuli.
Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga akisalimiana na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli mara baada ya kuwasili Chato.
Waziri Mkuu wa mstaafu wa Kenya Raila Odinga akiwa na Rais John Magufuli, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli pamoja na Mke wa Raila Odinga Bi. Ida Odinga wakisali kwenye makaburi ya familia ya Mhe. Rais Chato Mkoani Geita.
Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga akisalimiana na mama mzazi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Bi Suzana Joseph Magufuli mara baada ya kuwasili Chato Mkoani Geita.
Comments