Tuesday, April 05, 2016

KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA KATIBA NA SHERIA YATEMBELEA MAMLAKA YA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA SEKTA YA HIFADHI YA JAMII (SSRA)

 Mkurugenzi Mkuu wa SSRA Bi. Irene Isaka akitoa mada na maelezo mbalimbali kuhusu Mamlaka pamoja na Sekta nzima kwa wajumbe wa kamati ya Bunge ya kudumu ya Katiba na Sheria ilipotembelea ofisi za SSRA, Dar es salaam hivi karibuni. 
 Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu Katiba na Sheria wakiwa na uongoziwa SSRA pamoja na  viongozi  toka Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu ), wakati kamati hiyo ilipofanya ziara katika ofisi za SSRA.

 Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu) Mhe. Antony Mavunde akieleza jambo wakati wa kikao kilichofanyika kwenye ziara ya Kamati ya bunge ilipotembelea ofisi za SSRA, Kamati  inayoongozwa na Mh. Mohamed Omary Mchengerwa (pili kulia). 
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) akihojiwa na waandishi toka vyombo mbalimbali vya habari baada ya kikao kilichofanyika wakati kamati ya Bunge ya Kudumu ya Katiba na Sheria ilipotembelea Mamlaka hiyo. 
 Picha ya Pamoja ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Katiba na Sheria ikiongozwa na Mh.Mohamed Omary Mchengerwa aliyekaa (wa tatu kushoto) akifuatiwa na Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu) Mhe. Antony Mavunde. Kati ya waliosimama Mwenyekiti wa Bodi ya SSRA Bw. Juma Muhimbi (wan ne kulia) akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa SSRA Bi. Irene Isaka (kushoto) pamoja na menejimenti ya SSRA. 

No comments:

RAIS DKT. SAMIA AKUTANA NA UJUMBE WA JUKWAA LA MABUNGE LA NCHI ZA MAZIWA MAKUU (FP-ICGLR) IKULU NDOGO TUNGUU, ZANZIBAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Kiongozi wa Jukwaa la Mabunge la...