Waziri wa habari, michezo. Utamaduni na sanaa Mhe. Nape Nauye akimkabidhi mkuu wa Mkoa wa Kigoma ipad nne kwaajili ya maofisa habari waliopo kwenye halmashauri zote za Mkoa huo.Picha zote na Editha Karlo wa blog ya jamii, Kigoma
Mkuu wa kanda ya magharibi wa shirika la utangazaji(TBC) Kigoma Zablon Mafuru akimuonyesha waziri wa habari, michezo, utamaduni na sanaa Mhe. Nape Nauye vifaa vya matangazo vya shirika hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga akitoa taarifa ya mkoa kwa waziri wa habari,michezo,utamaduni Mhe Nape Nauye ambaye yupo. Mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku moja
Waziri wa habari, michezo, utamaduni na sanaa Mhe. Nape Nauye akipanda mti wa kumbukumbu katika viwanja vya shirika la utangazaji(TBC) Kigoma, akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya siku mmoja Mkoani hapo
Waziri wa habari, michezo, utamaduni na sanaa Mhe. Nape Nahuye akiongea na wadau wa wizara yake (ambao hawapo pichani) katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa Mkoa.
Waziri wa habari, michezo, utamaduni na sanaa Mhe. Nape Nauye akitia saini katika kitabu cha wageni ofisi za shirika la utangazaji(TBC) Kigoma
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia jenerali mstaafu Emanuel Maganga akimpokea waziri habari, michezo, utamaduni na sanaa Mhe Nape Nauye ofisi kwake leo
Comments