Wednesday, April 20, 2016

WAKALA WA NISHATI VIJIJINI REA WATOA MSAADA KWA WAHANGA WA MAFURIKO KIJIJI CHA KISANGA IRINGA

Mtendaji wa Kitongoji Bi sarah Mbilinyi akipokea taa hizo toka kwa Mkuu wa wilaya Iringa bwana Richard Kasesela.
Wakala wa Nishati Vijijini REA, wametoa msaada wa taa za kutumia mionzi ya jua katka kijiji cha Kisanga kitongoji cha Kiala; Wilaya ya Iringa Kitongoji hiki ni kile kilichokumbwa na mafuriko na kaya zaidi ya 100 kukosa mahala pa kuishi. Kijiji kiliamua kuwatengea eneo ambalo watajenga makazi mapya. Akitoa msaada huo Bi Jaina Msuya Afisa habari REA aliwaasa wananchi kutunza taa hizo na kuhakikisha zinachukua muda mrefu. Akipokea msaada huo Mkuu wa wilaya Iringa bwana Richard Kasesela alisema taa hizo zitasaidia kupunguza kutoa mwanga pia watoto wanaweza kujisomea usiku na hatari ya nyoka itapungua. REA wametoa taa zenye thamani ya Sh Mil 7.
Wananchi wa kitongoji hicho wanaendelea na shughuli za ufyatuaji matofali ili kujenga nyumba.
5Mkuu wa wilaya Iringa bwana Richard Kasesela akionesha jinsi Sola inavyotumika kuchajia simu.
4
23Picha ya pamoja.
Post a Comment