Thursday, April 21, 2016

Katibu Mkuu ACT wazalendo ang'atuka


Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Samson Mwigamba ambaye anakwenda masomoni.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Chama hicho zimeeleza kwamba Mwigamba anakwenda kusoma Shahada ya Udhamiri ya Biashara (MBA) katika Chuo Kikuu cha Kenyatta ambapo ataanza masomo mwezi Mei 2016.
Uongozi wa Chama cha ACT Wazalendo umeridhia maombi ya katibu huyo kwenda kusoma ambapo Chama kimempongeza kwa jitihada ambazo alizifanya katika kusimika mfumo wa chama tangu chama kianze mwaka 2014 mwezi Mei.
Aidha Chama kimempongeza Mwigamba kwa hatua yake ya kwenda masomoni jambo ambalo litamuongezea uzoefu na uwezo wa kuja kukitumikia chama siku za usoni.
Pia kufuatia hali hiyo Kamati ya Uongozi imeagiza kamati ya mafunzo na uchaguzi ianze mchakato wa kumpata katibu mkuu mwingine wa chama hicho kwa kuzingatia katiba ya chama hicho.
Kwa kutambua mchango wa Mwigamba katika chama hicho ataagwa rasmi April 25 ili kumtakia masomo mema. SOURCE:EATV
Post a Comment