Monday, April 04, 2016

RAIS MAGUFULI AAHIRISHA SHAMRASHAMRA ZA MUUNGANO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
NEMBO YA TAIFATAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha Shamrashamra za maadhimisho ya siku ya Muungano kwa mwaka huu, ambayo huadhimishwa kila tarehe 26 ya Mwezi Aprili, na badala yake ameelekeza kuwa siku hiyo itakuwa ya mapumziko kama kawaida, na watanzania waiadhimishe wakiwa majumbani kwao ama katika shughuli zao binafsi.
Kufuatia kuahirishwa kwa shamrashamra hizo, Rais Magufuli ameelekeza kuwa fedha zilizopangwa kutumika kwa ajili ya kugharamia Vinywaji, Vyakula, Gwaride, Halaiki, Burudani mbalimbali na Hafla ya usiku ambazo ni zaidi ya shilingi Bilioni 2, zitumike kuanzisha upanuzi wa barabara ya “Mwanza – Airport” katika eneo linaloanzia Ghana Quaters hadi Uwanja wa Ndege wa Mwanza.
Barabara hiyo inafanyiwa upanuzi ili kukabiliana na kero ya msongamano mkubwa wa magari ambao unaathiri shughuli za kila siku za wananchi.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Chato
04 April, 2016

No comments: