NAIBU KATIBU MKUU BALOZI SIMBA AFUNGUA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI WIZARA YA MAMBO

nd1
Naibu Katibu Mkuu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba (kushoto), Katibu wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo, Amani Mashaka (katikati), anayefuata ni Katibu Msaidizi wa Baraza hilo, Jenita Ndone wakiwaongoza wajumbe wa Baraza hilo kuimba wimbo wa mshikamano daima kabla ya Naibu Katibu Mkuu kufungua kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
nd2
Naibu Katibu Mkuu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kabla ya kufungua mkutano wa siku moja wa baraza hilo uliofanyika katika Ukumbi wa Jeshi la Magereza, Ukonga, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake Balozi Simba aliwataka watumishi wa wizara yake wafanye kazi kwa bidii ili kuiletea maendeleo wizara hiyo.
nd3
Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Jeshi la Polisi, Arcado Nchinga akichangia mada katika kikao cha Baraza hilo kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam. . Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
nd4
Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakimsikiliza kwa makini Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Hassan Simba (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza na wajumbe hao katika Mkutano wa Baraza hilo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Comments