Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Ocean Road, Dk. Julius Mwaiselage (katikati) akiwa na wajumbe wa Bunge kamati ya Maendeleoya Jamii walipotembelea jengo jipya la taasisi hiyo linalojengwa kwa ajili ya kufunga mashine za mionzi
Mbunge Mbeya Mjini kwa tiketi ya CHADEA, Mh. Joseph Mbilinyi 'Sugu (Kulia) akiwa na wajumbe wengine wakitoka katika kuangalia jengo maalum linalojengwa kwa ajili ya kufungwa mashine za mionzi za kupimia ugonnjwa wa saratani.
Kamati ya Bunge ya Kudumu Huduma za Maendeleo ya Jamii mapema leo Aprili 5.2016 imetembelea Taasisi ya Saratani Ocean Road na kujionea uendeshaji unaoendelea katika taasisi hiyo ikiwemo pia kuangalia jengo maalum litakalowekwa mitambo ya mionzi ya taasisi hiyo.
Kamati hiyo inaongozwa na Mwenyekiti wake Mh. Peter Serukamba (Mbunge) pamoja na wajumbe mbalimbali wa kamati huku wakibaini changamoto ikiwemo ukosefu wa dawa zinazoikabili taasisi hiyo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Dk. Julius Mwaiselage katika taarifa yake kwa Kamati hiyo aliweza kubainisha changamoto mbalimbali zinazoikabili Ocean Road ikiewemo suala hilo la madawa na bajeti wanayoomba Serikali kwani uendeshaji ni mkubwa na kiwango wanachokipata ni kiasi wastani katika maobo yao hayo.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla aliweza kutoa maelezo ya Wizara yake hiyo ya Afya namna walivyojipanga kusaidia taasisi hiyo huku akiahidi kuyashughulikia matatizo yote kadri inavyowezekana.
Aidha, Wananchi wakiwemo ndugu wa wagonjwa wanaouza wagonjwa wao waliweza kumvamia Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla kwa lengo la kutaka kutatuliwa kero zao hasa suala la ukosefu wa dawa Hospitalini hapo ambapo walimuomba atatue tatizo hilo haraka.
Wananchi hao licha ya kupongeza huduma zitolewazo Hospitalini hapo na taasisi hiyo, tatizo lao kubwa ni ukosefu wa dawa kwani hali imekuwa ni ngumu kwa muda mrefu kwa wao kutafuta dawa nje ya taasisi hiyo na huko wanapozipata ni kwa bei kubwa.
Comments