Monday, April 04, 2016

MEMON JAMAAT YAIPIGA JEKI SHULE YA SEKONDARI MIKOCHENI

Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Mikocheni, Dar es Salaam na Meya Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akiwahutubia wanafunzi wa shule hiyo wakati wa hafla ya kupokea madawati 160 kutoka Taasisi ya kidini ya Memon Jamaat kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya elimu kwa wanafunzi wa shule hiyo. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Yusuf Esack Ayub, Mjumbe wa taasisi hiyo, Ayub Abdallah (kushoto) na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Salama Ndiyetabura (kulia).
C1Sehemu ya madawati 160 yaliyokabidhiwa na Taasisi ya kidini ya Memon Jamaat katika Shule ya Sekondari Mikocheni, Dar es Salaam leo (Aprili 4).
C2  Wanafunzi wa kidato cha kwanza na pili wa Shule ya Sekondari Mikocheni, Dar es Salaam wakimsikilza Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo na Meya Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akiwahutubia wakati wa hafla ya kukabihi madawati yaliyotolewa leo (Aprili 4) na Taasisi ya kidini ya Memon Jamaat.C4Mwenyekiti wa Taasisi ya kidini ya Memon Jamaat,Yusuf Esack Ayub akisaidiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Mikocheni na Meya Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda kukata utepe wakati wa hafla ya kukabidhi madawati 160 pamoja na vifaa mbalimbali kwaajili ya kusaidia maendeleo ya elimu kwa wanafunzi wa Shule hiyo, Dar es Salaam leo (Aprili 4). Wanaoshuhudia ni wanachama wa taasisi hiyo, walimu na wanafunzi shule hiyo.
C5Mwenyekiti wa Taasisi ya kidini ya Memon Jamaat, Yusuf Esack Ayub (kulia) akikabihi madawati 160 kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Mikocheni, Salama Ndiyetabura kwaajili ya kusaidia maendeleo ya elimu kwa wanafunzi wa shule hiyo Dar es Salaam leo (Aprili 4). Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo, Yusuph Mwenda, Mjumbe wa taasisi hiyo, Ayub Abdallah, Katibu wa taasisi hiyo, Ayub Esack (kushoto), waalimu na wanafunzi wa shule hiyo.
C6Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Mikocheni, Yusuph Mwenda (mwenye tai nyekundu) akizungumza jambo na Afisa Elimu (Taaluma) Mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Sunza baada ya kupokea Printer na madawati 160 kutoka Taasisi ya kidini ya Memon Jamaat kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya elimu kwa wanafunzi wa shule hiyo, jijini leo (Aprili 4). Kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Salama Ndiyetabura.
(Picha zote na Mpigapicha Wetu).
……………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu,
TAASISI ya kidini ya Memon Jamaat imekabidhi msaada wa madawati 160, Printer pamoja kuweka mfumo wa umeme (wiring) katika Shule ya Sekondari Mikocheni, Dar es Salaam vikiwa na thamani ya shilingi milioni 22.3.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Yusuf Esack Ayub alisema msaada huo ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha sekta ya elimu kupitia mpango wake wa elimu bure.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa licha ya Serikali kuanzisha mpango wa elimu bure nchini haiwazuii wao kama wadau wa elimu kusaidia maendeleo ya elimu nchini na hivyo kuamua kuisaidia shule hiyo pekee ya Serikali ya Sekondari katika Kata ya Mikocheni ili iweze kuleta ushindani mkubwa wa kielimu.
“Sisi tumeitikia ilani ya Rais wetu John Magufuli ya elimu bure na kuamua kuleta msada huu utakaokuwa endelevu shuleni hapa. Pia tutafanya mpango wa kuleta vifaa vya maabara ili tupate wataalamu wazuri kutoka shule hii.” Alisema Mwenyekiti uhuyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo na Meya Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda aliwashukuru wafadhili hao na kuomba wadau wengine wa elimu kujitokeza kuisaidia shule hiyo katika maeneo mengine ya kielimu.
Mwenda alisema kuwa misaada kama hiyo sit u inasaidia maendeleo ya shule ila inasaidia pia hata familia za hali ya chini ambazo ndizo zenye watoto wanaosoma katika shule hizo na kusisitiza kuwa wadau wa elimu wana wajibu wa kuunga mkono kauli ya Rais John Magufuli ya elimu bure kwa kusaidia maeneo mbalimbali ikiwemo vifaa vya shule.
“Tunashukuru Memon Jamaat kwa moyo wenu mliokuwa nao wa kuja kuisaidia shule hii. Mnachokifanya nyie kwanza mnawasaidia watoto wa kitanzania, hizi shule za Kata wanaosoma ni watoto wa watu wa kawaida sana, huwezi kwenda kuwasaidia kwenye nyumba zao, ukisaidia kuboresha mazingira ya elimu unawasaidia wao na familia zao, lakini unaisaidia nchi itakuja kupata wataalamu wazuri watakaokuja kuisaidia Tanzania, mi nawashukuru sana.” Alisema Yusuph Mwenda.
Mwenyekiti huyo alizitaka taasisi nyingine kujitokeza kusaidia shule hiyo pamoja na nyingine za Serikali ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Srikali ya Rais John Magufuli za kuboresha sekta ya elimu nchini.
Naye Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Salama Ndiyetabura alisema kuwa baada ya kuwekewa mifumo ya umeme na taasisi hiyo, walifanya mawasiliano na Tanesco na kuwaahidi kuleta mkaguzi wao na kuwaingizia umeme mara moja.
Post a Comment