Tuesday, April 26, 2016

PROF. MBARAWA ATOA WIKI MBILI BARABARA YA MORROCO-MWENGE


 Mafundi wa kampuni ya Estim Construction wakiendelea
na Ujenzi wa barabara ya Mwenge –Morocco KM 4.3 ambayo ni sehemu ya Barabara ya
Morocco –Mwenge-Tegeta.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS
akimuonyesha Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano kazi ya ujenzi wa
mifereji pembezoni mwa Barabara ya Morocco-Mwenge inavyoendelea.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa
Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini
TANROADS Eng.Patric Mfugale kuhusu kukamilika kwa upanuzi wa barabara ya Morocco-Mwenge
KM 4.3.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa
Makame Mbarawa(Watatu kushoto) akifafanua jambo kwa wafanyakazi  wa mamlaka ya hali ya hewa nchini (Hawapo
pichani) huku Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt.Agness Kijazi ( Watatu kulia)
akifuatilia kwa makini.
 Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa nchini Dkt
Agness Kijazi akimuonyesha Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano moja ya
ramani zinazotumika katika masuala ya utabili wa hali ya hewa.
 Mtaalamu wa maswala ya hali ya hewa nchini Didasian
Kankesha akifuatilia utabiri kabla ya uhakiki na kuutangaza kwa wadau.
 Mtaalam wa kusoma utabiri wa hali ya hewa Hellen Msemo
akimuonyesha Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano namna taarifa za utabiri
wa hali ya hewa zinavyorekodiwa na kutumwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari.
Post a Comment