Wednesday, November 04, 2015

DK. JOHN POMBE MAGUFULI AMPOKEA TB JOSHUA KUTOKA NIGERIA, KUSHUHUDIA KUAPISHWA KWAKE

Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiongozana na Temitope Balogun Joshua maarufua kama TB Joshua Mkuu wa Kanisa la (Synagogue Church of All Nations a religious organisation) la Nigeria,  wakati alipomlaki kwenye uwanja wa Ndege wa J.K. Nyerere International Airport jijini Dar es salaam.
TB Joshua amekuja nchini kushuhudia kuapishwa kwa Dk. John Pombe Magufuli atakayeapa kuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania akimrithi Rais anayemaliza muda wake Dk. Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kuongoza nchi kwa miaka 10 .
Dk. John Pombe Magufuli ataapishwa kwenye uwanja wa Taifa wa zamani Novemba 5 Alhamisi mwaka huu jijini Dar es salaam na kushuhudiwa na wananchi vyombo vya ulinzi na usalama, viongozi kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika na Ulaya wakiwemo mabalozi mbalimbali. T.B. Joshua akiwa katika picha ya pamoja na Edward Lowassa.
Post a Comment